Economist SHILLA Jr.
88 subscribers
About Economist SHILLA Jr.
ONGEZA MAARIFA, INUA THAMANI YAKO NA IMARISHA KIPATO CHAKO
Similar Channels
Swipe to see more
Posts
HALI YAKO YA MADENI IKOJE, JIBU MASWALI YAFUATAYO UWEZE KUJUA MADENI YAKO YAMEFIKIA HATUA GANI: Kwa hali ya kawaida madeni yanapaswa kuwa himilivu kulingana na ukubwa wa KIPATO CHAKO. Uhimilivu wa madeni ni kwamba unaweza kurejesha MIKOPO au kulipa madeni yote bila kuathiri ubora wa maisha yako na familia yako. Ukitaka kubaini madeni yako yamefikia kiwango Cha kukutesa na kuathiri maisha yako kwa ujumla, jiulize maswali yafuatayo; 1. Madeni uliyonayo yanakufanya kukosa furaha? 2. Je, msukumo kutokana na madeni uliyonayo yanaathiri kazi yako na shughuli zako za kila siku? 3. Je, madeni uliyonayo yanaharibu heshima yako? 4. Je, madeni yanakufanya usijifikirie wewe zaidi? 5. Je, umewahi kutoa taarifa za uongo ili upate mkopo? 6. Je, umewahi kutoa ahadi zisizohalisi kwa wanaokukopesha? 7. Je, msukumo wa madeni uliyonayo yanakufanya kutokujali masuala ya familia yako? 8. Je, umewahi kuhofia mwajiri wako, familia yako au marafiki kujua kuhusu ukubwa wa madeni yako? 9. Ukiwa katika changamoto za kifedha, unajisikia ahueni zaidi juu ya kukopa? 10. Je, msukumo wa madeni uliyonayo yanasababisha kukosa usingizi? 11. Je, msukumo wa madeni uliyonayo yanasababisha kutumia pombe na madawa? 12. Je, umewahi kukopa pesa bila kujiridhisha vya kutosha kuhusu kiwango cha riba unayotakiwa kukopa? 13. Je, wakati wote unategemea tathmini hasi ukitakiwa kufanyiwa tathmini ya uwezo wako wa kukopesheka? 14. Je, umewahi kuweka ratiba ngumu kwa ajili ya kulipa madeni ili kuondokana na msukumo wa madeni? 15. Je, unaweza kutolea maelezo madeni yako na kujiambia mwenyewe kwamba una madeni mengi na kipindi ambacho ukiweza kurejesha madeni yataisha ndani ya kipindi kifupi? KAMA KUNA JAMBO UMEJIFUNZA TUAMBIE KWENYE COMMENT NA USIACHE KUSAMBAZA (SHARE) ANDIKO HILI. Book huduma zetu; 1. Ushauri wa ana kwa ana bila kujumuisha maandalizi ya NYARAKA n.k (120,000/=); 2. Ushauri kupitia simu pekee (40,000/=); 3. Kuandaa NYARAKA ya mpango wa biashara au mradi (150,000 - 500,000/=) 4. Kuzungumza katika tukio (250,000/= bila kujumuisha gharama za kujikimu kama zipo); 5. Kufundisha mada mbalimbali (25,000/=@mshiriki au 250,000/= kwa siku, washiriki wasiozidi 10); Kwa mawasiliano na mialiko yote ya kibiashara piga simu 0672619660 au baruapepe [email protected].
FAHAMU KUHUSU URAIBU WA KUTUMIA PESA KATIKA UNUNUZI WA BIDHAA NA TIBA YA TATIZO HILO: Hii ni hali ambayo mtu anajisikia uhitaji usio na udhibiti wa kufanya manunuzi au kutumia pesa kwa ajili yako au kwa wengine. Tafiti zinaonesha kwamba mtu mmoja kati ya watu saba (7) ana uraibu wa kutumia pesa au kununua bidhaa ambazo kuna uwezekano hawatazitumia hapo baadaye. Tunafahamu kwamba sisi wote huwa kuna wakati tunatumia pesa zaidi ya kiwango tulichopanga kutumia katika manunuzi ya bidhaa tusizohitaji, lakini ukiwa na tabia ya kufanya manunuzi zaidi ya kipato chako, utambue una tatizo la uraibu wa kufanya manunuzi. Kama una tatizo kama hili usiogope kuomba msaada ili upone kabla hujaharibu uhusiano wako na watu wengine na kutumbukia katika dimbwi la madeni sugu. Viashiria kwamba una tatizo la uraibu wa manunuzi na matumizi ni pamoja na: Mara nyingi kununua bidhaa ambazo huzihitaji; Kila mara unafanya manunuzi au kutumia pesa zaidi ya uwezo wako wa kununua; Kila mara unanunua vitu kwa mkopo na kulimbikiza madeni; na Unanunua vitu ili ujisikie vizuri tuu. Unaweza kutafuta tiba ya tatizo la uraibu wa matumizi na manunuzi kwa kufanya yafuatayo: Tafuta tiba ya mtu mmoja mmoja au kundi, au ushauri wa kifamilia au tafuta makundi saidizi; Tafuta uhauri wa kifedha ili kusimamia mdeni yako na kupanga bajeti ya matumizi ikijumuisha Bajeti na mpango wa kuweka akiba; Weka vikwazo vya pesa yako kwa kubeba pesa ya kutosha kufanya manunuzi ya kila siku na dharura tuu; Kaa mbali na vishwawishi vya kufanya manunuzi yasiyo ya lazima na kununua bidhaa usizozihitaji. Katika kuepuka vishwawishi hivyo, jiulize maswali yafuatayo kabla ya kununua bidhaa yoyote; Je, unakihitaji?, kwanini sasa?, Unaweza kupata chenye bei nafuu?, je, ukinunua utapata faida gani?; Tembelea maduka mbalimbali kujua bei ya bidhaa, na kama utaweza subiri kama siku moja kabla ya kununua ili uweze kufikiri zaidi kuhusu ununuzi huo; Usiruhusu uraibu wa kutumia pesa au kufanya manunuzi uharibu maisha yako. Dhibiti kwa kutafuta ushauri wa kitaalam na kuepuka mazingira au hali inayoweza kukufanya kunumia pesa zaidi na hovyo. KAMA KUNA JAMBO UMEJIFUNZA TUAMBIE KWENYE COMMENT NA USIACHE KUSAMBAZA (SHARE) ANDIKO HILI. Book huduma zetu; 1. Ushauri wa ana kwa ana bila kujumuisha maandalizi ya NYARAKA n.k (120,000/=); 2. Ushauri kupitia simu pekee (40,000/=); 3. Kuandaa NYARAKA ya mpango wa biashara au mradi (150,000 - 500,000/=) 4. Kuzungumza katika tukio (250,000/= bila kujumuisha gharama za kujikimu kama zipo); 5. Kufundisha mada mbalimbali (25,000/=@mshiriki au 250,000/= kwa siku, washiriki wasiozidi 10); Kwa mawasiliano na mialiko yote ya kibiashara piga simu 0672619660 au baruapepe [email protected].
UHUSIANO WA MAARIFA YA KIFEDHA NA MPANGO WA KUSTAAFU KWA WATUMISHI WA UMMA: Mpango binafsi wa kustaafu ni hatua inayojumuisha masuala ya uwekezaji au uwekaji akiba kwa lengo la kuwa na kipato cha kutosha kipindi mtumishi anapostaafu. Mchakato huu wa kupanga mpango wa kustaafu hufanywa na mtumishi miaka michache baada ya kuajiriwa au angalau miaka 15 kabla ya kufikia kipindi cha kustaafu. Hata hivyo, watumishi wengi wanapitia changamoto nyingi hasa katika eneo la usimamizi wa fedha wanazopata na katika kufanya maamuzi ya kifedha katika maisha yao. Hali hiyo, inasababisha watumishi kushindwa kufanya maandalizi ya kustaafu kwa wakati au kutokujiandaa kabisa kipindi cha utumishi wao. Tafiti nyingi zimebainisha kwamba usimamizi mbovu wa fedha na maamuzi ya kifedha yasiyo sahihi yanasababishwa na watumishi wengi kukosa Elimu, Maarifa na Uelewa wa masuala mbalimbali ya kifedha. Kwanini tunajifunza kuhusu masuala ya maarifa ya kifedha na mpango wa kustaafu? • Kipindi mtumishi anapostaafu kipato chake hupungua na hali hiyo huleta madhara kwa mstaafu. Aidha, watumishi wengine hustaafu wakiwa na madeni mengi, hivyo kipato kinachoingia kushindwa kutosheleza kulipa madeni na kugharamia matumizi ya kila siku ya familia. • Mifuko ya hifadhi ya jamii haitoi kipato kinachotosheleza kugharamia matumizi kwa watumishi walio wengi kulingana na mtindo wao wa maisha (matumizi makubwa kuliko kipato). Hivyo, mpango wa kustaafu wa ziada (Kuwa na akiba, kuwa na miradi inayoingiza kipato, kupunguza matumizi n.k) ni muhimu kuhakikisha wastaafu wanaishi maisha ya staha wanapostaafu. • Kuwekeza katika kutafuta maarifa ya kifedha imethibitishwa kwamba ni muhimu na ina matokeo chanya katika eneo la jinsi ya watumishi wanavyopanga kuhusu kustaafu kwao na baadaye kuwa na uwezo wa kuwa na rasilimali za kutosha wanapostaafu. • Kuna athari hasi nyingi za kutokuwa na maarifa ya kifedha kama vile Msongo wa kifedha (Financial Stress) unaoweza kumuathiri mtumishi kwa kuwa mtoro kazini, tija inapungua, haridhiki anapofanya malipo, anatumia muda wa kazi kushughulikia changamoto zake za kifedha, Madeni ya Kupindukia, Tabia duni za kifedha kushindwa kufanya makisio sahihi ya kipato na gharama, kutokuwa na fedha ya dharura, kununua bidhaa na huduma kwa mkopo na kutokuwa na mipango na bajeti ya mwaka, miezi sita, n.k. • Maisha ya uzeeni au baada ya kustaafu yanahusisha changamoto nyingi za kiafya, hivyo usipoweka mpango thabiti wa maisha yako baada ya kustaafu utapata changamoto sana kugharamia matibabu n.k. KAMA KUNA JAMBO UMEJIFUNZA TUAMBIE KWENYE COMMENT NA USIACHE KUSAMBAZA (SHARE) ANDIKO HILI. Book huduma zetu; 1. Ushauri wa ana kwa ana bila kujumuisha maandalizi ya NYARAKA n.k (120,000/=); 2. Ushauri kupitia simu pekee (40,000/=); 3. Kuandaa NYARAKA ya mpango wa biashara au mradi (150,000 - 500,000/=) 4. Kuzungumza katika tukio (250,000/= bila kujumuisha gharama za kujikimu kama zipo); 5. Kufundisha mada mbalimbali (25,000/=@mshiriki au 250,000/= kwa siku, washiriki wasiozidi 10); Kwa mawasiliano na mialiko yote ya kibiashara piga simu 0672619660 au baruapepe [email protected].
KILA SIKU JIULIZE MASWALI KUMI (10) ILI UWEZE KUTAFAKARI NA KUAMUA KUWEKA MIKAKATI THABITI ILI USONGE MBELE KIFIKRA NA KIMAENDELEO: Katika maisha kuna maswali mengi tunapaswa kujiuliza mara kwa mara kwa ajili ya kutafakari na kujitathmini wenyewe kwa lengo la kusonga mbele kimaendeleo. Leo nimepata kibali cha kukuletea maswali kumi (10) ambayo kwa namna moja au nyingine ukitumia muda wako kujiuliza, kutafakari na kutafuta majawabu basi yatakusaidia kupiga hatua moja mbele kifikra na kimaendeleo. Maswali haya ni kama ifuatavyo; 1. Je, tabia zako za kila siku zinakusaidia katika kusimamia pesa zako vizuri katika uwekaji wa akiba na uwekezaji au ni chanzo cha kufuja na kutapanya pesa hovyo? 2. Je, unafahamu unahitaji kiasi gani cha fedha kwa ajili ya matumizi yako kwa kipindi cha mwezi mmoja, miezi mitatu, miezi sita au mwaka mzima? 3. Je, unajua fedha (kipato) zako unazoingiza kwa mwaka mzima huwa zinatumika wapi na kiasi gani kinatumika katika maendeleo na kiasi gani kinatumika katika matumizi ya kawaida? 4. Je, unaweza kurejea katika hali yako ya sasa kwa haraka (uhimilivu) kipindi unapopatwa na matatizo au changamoto za kifedha? 5. Je, umewahi kujiuliza, marafiki na jamaa waliokuzunguka ni faida au hasara kwako?. Wanakusaidia kuongeza kipato au kuongeza matumizi na madeni? 6. Je, kiwango cha akiba ya fedha ulichonacho kinatosha kuendesha maisha yako kwa kipindi cha miezi mingapi iwapo utakosa kazi ya kukuingizia kipato, mfano umeachishwa kazi n.k? 7. Je, kiwango cha madeni ulichonacho ni himilivu au madeni yamesababisha kutoaminika kwa marafiki na ndugu zako?. 8. Je, mwenza uliyenaye ni chanzo cha migogoro ya kifedha ndani ya ndoa au yeye ni msaada mkubwa katika usimamizi wa fedha ikijumuisha matumizi mazuri ya fedha, uwekaji akiba na uwekezaji? 9. Je, unapoenda kufanya manunuzi ya bidhaa sokoni unatumia mbinu gani ili uweze kununua biadhaa unazohitaji kwa bei nafuu na kwa kuzingatia mahitaji halisi au unapoenda sokoni unanunua bidhaa chache kwa bei kubwa au ukanunua bidhaa usizozihitaji kwa wakati huo. 10. Je, mali ulizonazo iwe fedha, nyumba, viwanja, mashamba n.k zinafikia thamani ya kiwango gani? Je kwa sasa unao utajiri (net worth) wa kiwango gani ukitoa madeni uliyodaiwa? Book huduma zetu; 1. Ushauri wa ana kwa ana bila kujumuisha maandalizi ya NYARAKA n.k (120,000/=); 2. Ushauri kupitia simu pekee (40,000/=); 3. Kuandaa NYARAKA ya mpango wa biashara au mradi (150,000 - 500,000/=) 4. Kuzungumza katika tukio (250,000/= bila kujumuisha gharama za kujikimu kama zipo); 5. Kufundisha mada mbalimbali (25,000/=@mshiriki au 250,000/= kwa siku, washiriki wasiozidi 10); Kwa mawasiliano na mialiko yote ya kibiashara piga simu 0672619660 au baruapepe [email protected].
ATHARI ZA CHANGAMOTO BINAFSI ZA KIFEDHA KWA WAFANYAKAZI MAHALI PA KAZI: Masuala ya kifedha yana uhusiano wa karibu sana na changamoto ya msongo wa mawazo kwa mfanyakazi kwani ndiyo sababu kubwa inayoleta msongo wa mawazo kwa watu wengi. Mara nyingi watu wanakuwa na hofu juu ya uwezo wao wa kifedha hasa kipindi wanapowaza kuhusu marejesho ya mikopo, maandalizi ya kustaafu au kugharamia bili za kila mwezi. Hofu hii inakuwepo hata kwa familia ambazo mume na mke wote wanaingiza kipato, kwa sababu ni ukweli kwamba kipato hakijawahi kutosheleza mahitaji ya kila siku. Wafanyakazi waliowengi wanapitia changamoto nyingi za kifedha hasa katika eneo la usimamizi wa fedha wanazopata na kufanya maamuzi sahihi ya kifedha. Kwa mujibu wa utafiti uliohusisha mameneja wa rasilimaliwatu 300, asilimia 32 yao walibainisha kwamba matatizo au changamoto binafsi za kifedha kwa wafanyakazi ni changamoto kubwa isiyopewa kipaumbele na waajiri mbalimbali mahali pa kazi. Changamoto za kifedha kwa wafanyakazi zinasababishwa na wafanyakazi wengi kukosa uelewa, elimu na maarifa ya kifedha ambapo hushindwa kusimamia fedha wanazoingiza na kufanya maamuzi ya kifedha yasiyo sahihi. Maamuzi ya kifedha yasiyo sahihi yanahusisha kukopa mikopo kausha damu yenye riba kubwa, kufanya uwekezaji katika eneo lisilo na faida n.k Hali hiyo, humletea mfanyakazi msongo wa mawazo mahali pa kazi na kusababisha mfanyakazi kuwa mtoro kazini, kuwa na ufanisi hafifu kazini, kupata maradhi kama shinikizo la moyo, kutokuridhika na malipo ya mwajiri na kutumia muda wa kazi kufanya shughuli binafsi ba kuongeza kipato n.k. Changamoto za kifedha kwa wafanyakazi hazitatuliwi kwa kuongeza viwango vya mishahara au posho bali Taasisi husika kuwajengea uwezo watumishi wake kwa kutoa mafunzo ya usimamaizi wa fedha na uwekezaji. Baadhi ya Taasisi zina utaratibu wa kutoa mafunzo na semina mbalimbali kuhusu usimamizi wa fedha na uwekezaji, mikopo na madeni, kupanga bajeti na kujiandaa kustaafu. Ingawa kwa waajiri waliowengi jambo hili halifanyiki ama kwa kutokutambua umuhimu wake ama kukosa rasilimali fedha kwa ajili ya kutekeleza jambo hilo. Tunakuachia swali, je mwajiri wako anafanya semina na mafunzo kuhusu usimamizi wa fedha na maandalizi ya kustaafu? Ukiacha kuwajengea uwezo watumishi, mfanyakazi anaweza kushugulikia changamoto za kifedha kuweka utaratibu wa kuweka akiba, kuwa na bajeti na kuanza kujiandaa kustaafu mapema. Ili kufanikisha haya, mfanyakazi anapaswa kupata uelewa, elimu na maarifa ya kifedha kupitia usomaji wa vitabu mbalimbali, kupitia majukwaa ya mitandao ya kijamii, kupata mtaalam mshauri au kuhudhuria semina na mafunzo mbamlimbali yanayotolewa na kampuni au watu mbalimbali. Maarifa ya kifedha yatamsaidia kufanya maamuzi bora kuhusu masuala ya kifedha na kupunguza msongo wa mawazo. Book huduma zetu; 1. Ushauri wa ana kwa ana na ufuatiliaji wake bila kujumuisha maandalizi ya nyaraka n.k (Shs. 120,000/=); 2. Ushauri kupitia simu pekee (Shs. 40,000/=); 3. Kuandaa nyaraka ya mpango wa biashara au mradi (Shs. 150,000 - 500,000/=) 4. Kuzungumza katika tukio/semina (Shs. 250,000/= bila kujumuisha gharama za kujikimu kama zipo); 5. Kufundisha mada mbalimbali (Shs. 25,000/=@mshiriki au Shs. 250,000/= kwa siku, washiriki wasiozidi 10); Kwa mawasiliano na mialiko yote ya kibiashara piga simu 0672619660 au baruapepe [email protected].
MAARIFA NI MAANDISHI NA MAWAZO MAPYA YAPO KATIKA VITABU: UKIJIFUNZA ZAIDI UTAINGIZA PESA ZAIDI; Katika utaratibu wangu wa kila siku wa kusoma vitabu, makala na majarida mbalimbali nilibaini kwamba karibu asilimia 90 ya matajiri duniani ni matajiri wa kizazi cha kwanza. Matajiri hawa utajiri wao sio wa kurithi bali wametengeneza wenyewe. Aidha, tafiti nyingi zinabainisha kwamba karibu matajiri wote hawa wa kizazi cha kwanza walipata mawazo ya biashara na kufanikiwa katika biashara kwa kusoma vitabu na maandiko mbalimbali. Hili linathibitishwa na ukweli kwamba MAWAZO MAPYA HUPATIKANA KATIKA VITABU VYA ZAMANI. Aidha, nilibaini kwamba matajiri hawa kwa mwaka husoma wastani wa vitabu 50, ambapo kwa kwa wiki wanasoma angalau kitabu kimoja. Swali linabaki kwako, unasoma vitabu vingapi kwa siku, kwa wiki, kwa mwezi na kwa mwaka? na Je, utaweza kusoma vitabu 50 kwa mwaka, jaribu na anza sasa, kila kitu kinawezekana hapa duniani. Vilevile, nilibaini kwamba matajiri hawa hawapendelei kusoma vitabu vya Riwaya na Tamthiliya bali husoma vitabu vyenye msaada katika biashara zao wanazofanya. Kwa mfano, matajiri wanasoma zaidi vitabu kuhusu MASOKO, TEKNOLOJIA, USIMAMIZI WA FEDHA, KUWEKA AKIBA, UWEKEZAJI, MAWASILIANO YA KIBIASHARA, USIMAMIZI WA MIRADI n.k. Swali linabaki kwako, unapendelea kusoma vitabu vya aina gani na vyenye maudhui gani? Ukweli ni kwamba maarifa yanayopatikana katika vitabu au maandishi yana msaada mkubwa, kwa sababu, unaweza kuwa na ujuzi fulani, mfano ujuzi wa kufuga kuku, kilimo cha nyanya, n.k sasa jiulize kama huna maarifa kuhusu masoko, uwekezaji, fedha, utawezaje kufanya KILIMO BIASHARA? Ukiweza kupata pesa kupitia maarifa, utabaini kwamba kuna uhusiano katika kujifunza na kuingiza kipato, nikimaanisha kwamba UKIJIFUNZA ZAIDI UTAINGIZA PESA ZAIDI. Dhana hii ni ngumu kueleweka, lakini anza kujifunza leo, uweze kuwa shuhuda wa mabadiliko na mafanikio katika biashara yako au shughuli unayofanya. Kuna faida nyingi za kujifunza zaidi, ikiwemo kuongeza maarifa na uelewa kuhusu jambo fulani, na kukusaidia katika shughuli zako. Aidha, unapo ongeza maarifa unaweza kufanya shughuli zako kwa ufanisi zaidi na kuongeza tija. Vilevile, ukiwa na uelewa wa mambo mengi unaongeza kujiamini ambapo utakuwa na uwezo na utulivu katika kufanya majadiliano ya kibiashara na wakati wa kufanya mawasilisho katika hadhara mbalimbali. Mwisho kabisa narudia Tena MAARIFA YAMEFICHWA KATIKA MAANDISHI NA MAWAZO MAPYA YAMEWEKWA KATIKA VITABU VYA ZAMANI. Kwa hiyo, usichoke kujifunza kila siku, na kwa msaada zaidi usisite kupata ushauri kutoka kwa wataalam washauri. Book huduma zetu; 1. Ushauri wa ana kwa ana na ufuatiliaji wake bila kujumuisha maandalizi ya nyaraka n.k (Shs. 120,000/=); 2. Ushauri kupitia simu pekee (Shs. 40,000/=); 3. Kuandaa nyaraka ya mpango wa biashara au mradi (Shs. 150,000 - 500,000/=) 4. Kuzungumza katika tukio/semina (Shs. 250,000/= bila kujumuisha gharama za kujikimu kama zipo); 5. Kufundisha mada mbalimbali (Shs. 25,000/=@mshiriki au Shs. 250,000/= kwa siku, washiriki wasiozidi 10); Kwa mawasiliano na mialiko yote ya kibiashara piga simu 0672619660 au baruapepe [email protected].
JENGA TABIA YA KUTAFUTA ELIMU, MAARIFA NA UJUZI, HUKO NDIKO MWANGA WA MAFANIKIO ULIKOJIFICHA: Katika Dunia ya Leo, usijidanganye kufanya maamuzi ya kifedha mfano Uwekezaji bila kuwa na taarifa muhimu katika eneo unalotaka kuwekeza, vinginevyo utakuwa unajipanga kushindwa. Katika Dunia ya Leo, ukiwa na taarifa sahihi na zilizokamilika basi unaweza kufanya maamuzi sahihi kwa karibu asilimia 99.9 na utakuwa na uhakika wa kufanikisha malengo Yako. Katika Dunia ya Leo, wawekezaji wakubwa na wadogo wanawekeza fedha, nguvu na akili zao katika kufanya tafiti za fursa, tafiti za masoko na bei, tafiti za tabia za walaji n.k ili waweze kufanya maamuzi yaliyo sahihi katika uwekezaji wao. Katika Dunia ya Leo, ni wazi na ukweli kwamba katika uwekezaji Kuna vihatarishi vingi na uwezekano mkubwa wa malengo kutokufikiwa kwa sababu mbalimbali kama Hali ya uchumi, mfumuko wa bei, kudorora kwa soko n.k, hivyo kuna umuhimu mkubwa kuwekeza katika kutafuta maarifa, elimu, na ujuzi sambamba na kutafuta taarifa muhimu kupitia tafiti mbalimbali ili uweze kuyafikia malengo yako katika uwekezaji wako. Katika Dunia ya Leo, ukweli ni kwamba unaweza kuwa na elimu Yako katika eneo Fulani, lakini usiwe na maarifa kuhusu biashara, ukakosa maarifa kuhusu masoko na mbinu za majadiliano ya kibiashara na wadau wako n.k, kwa maana hiyo, usiogope kuomba ushauri, kuuliza, kusoma makala mbalimbali, kusoma vitabu, kupitia YouTube na google n.k ili uweze kupata maarifa, elimu na ujuzi unao uhitaji. Katika Dunia ya Leo, unaweza ukasomea ufugaji wa kuku, lakini kumbuka kuwa unahitaji ujuzi, elimu, na maarifa ya kifedha, uwekezaji, masoko, utawala n.k ili uweze kufanikiwa katika biashara Yako. Pamoja na mwelekeo wa Dunia hii, bado hapa kwetu Tanzania, watu hawana utamaduni wa kutafuta ushauri, taarifa, maarifa, ujuzi na elimu katika maeneo wanayotaka kuwekeza au waliyowekeza. Ukweli ni kwamba mafanikio katika uwekezaji au biashara hayana bahati inayotoka pasipojulikana bali ni lazima ufanye uwekezaji wenye tija. Na tija itapatikana kama ukiwekeza kutafuta haya tunayoyaongelea Leo!! Katika Dunia, ya Leo, usiogope kupata ushauri kutoka kwa wataalam ambao wanawekeza muda, akili na fedha kwa ajili ya kuwashauri watu katika maeneo mbalimbali ya utaalam wao. Watu hawa, Wana msaada sana. Usiogope gharama, japo kuna gharama katika ushauri unaopewa kwa kuwa tuna uhakika utaleta matokeo kwako. Mwisho kabisa, katika Dunia ya Leo, hakuna njia ya mkato kuelekekea mafanikio katika shughuli yoyote unayofanya. Kwa hiyo, nasisitiza tena kwamba JENGA TABIA YA KUTAFUTA ELIMU, MAARIFA NA UJUZI, HUKO NDIKO MWANGA WA MAFANIKIO ULIKOJIFICHA. Book huduma zetu; 1. Ushauri wa ana kwa ana bila kujumuisha maandalizi ya NYARAKA n.k (120,000/=); 2. Ushauri kupitia simu pekee (40,000/=); 3. Kuandaa NYARAKA ya mpango wa biashara au mradi (150,000 - 500,000/=) 4. Kuzungumza katika tukio (250,000/= bila kujumuisha gharama za kujikimu kama zipo); 5. Kufundisha mada mbalimbali (25,000/=@mshiriki au 250,000/= kwa siku, washiriki wasiozidi 10); Kwa mawasiliano na mialiko yote ya kibiashara piga simu 0672619660 au baruapepe [email protected].
Huduma zetu ni pamoja na; MAFUNZO NA USHAURI; Usimamizi wa fedha, Uwekezaji, Kujiandaa kustaafu, Uwekaji akiba, Mikopo na jinsi ya kuondokana na madeni sugu, n.k, MAFUNZO NA USHAURI: Uanzishaji na uendelezaji wa biashara, Mipango ya biashara, Usimamizi wa biashara, utafutaji na utafiti wa masoko, Huduma kwa wateja, n.k. Walengwa wa huduma zetu ni pamoja na makundi mbalimbali kama vile: MTU MMOJA MMOJA, TAASISI, WAFANYAKAZI KATIKA TAASISI MBALIMBALI, VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI, WAFANYABIASHARA WADOGO, VIKUNDI/ JUMUIYA MBALIMBALI VYA KIJAMII, n.k. Mawasiliano na mialiko yote ya kibiashara ipitie kwa simu namba 0672619660 na baruapepe [email protected]. GHARAMAZ ZETU NI NAFUU SANA
MAFANIKIO KATIKA BIASHARA NI IMANI YA MTU ILIYOJIFICHA KATIKA KIPAJI NA BIDII YA KAZI: NIMEWAHI KUONA wafanya biashara ambao wanauza bidhaa moja kwa zaidi ya miaka 20 na wameweza kujikimu na kufanya maendeleo ya kiuchumi kulingana na kipato wanachoingiza. Wafanyabiashara hawa wanayo IMANI juu ya biashara zao kwamba zinaweza kuwatoa mahali kwenda mahali pengine pa juu zaidi. Wafanyabiashara hawa, huwa hawafikirii kuongeza biashara nyingine wala kupanua au kukuza biashara zao. Kwa mwenendo huo, utabaini kwamba wafanyabiashara hawa wanayo IMANI kubwa na biashara zao, wana AMINI katika VIPAJI vyao na wamewekeza BIDII katika biashara zao bila kuchoka. NIMEWAHI KUONA watu wanaofanya biashara kama FAHARI kwa jamii inayowazunguka, na biashara zao zimekuwa zikiwatesa, hawana MUDA wa usimamizi wa biashara, hakuna mgawanyo mzuri wa majukumu katika biashara zao kila mtu ni muuzaji au mhudumu au mhasibu. BIASHARA zinawaletea hasara kila kukicha lakini wanaogopa kufunga biashara kwa sababu wanataka kuiaminisha jamii inayowazunguka kwamba biashara zao zinaenda vizuri na zinawapa faida ili kulinda ufahari wao. Wakati mwingine hutumia kipato chao kingine kuboresha biashara zao kwa kununua bidhaa au malighafi ili biashara zao zisidorore tofauti na utaratibu kibiashara unaosisitiza biashara kujiendesha zenyewe. Watu hawa kwa maneno mafupi ni kwamba IMANI wanayo lakini hawana KIPAJI na BIDII katika kazi. NIMEWAHI KUONA watu ambao walianza biashara zao na mtaji mdogo katika biashara zao na wameweza kukuza au kupanua bishara zao na kuongeza maeneo ya uwekezaji wao ndani ya kipindi cha miaka mitano (5) hadi 10. Ukiwafuatilia watu hawa wanauwezo mkubwa wa kujenga mahusiano na wateja, wauza malighafi na watu wengine, lakini pia watu hawa wanatumia muda mwingi kuzitafuta fursa za biashara popote zilipo na kuwekeza haraka. Watu hawa wameweka utaratibu mzuri wa usimamizi wa biashara zao, kuanzia ununuzi wa bidhaa, mauzo, ukusanyaji wa mauzo, madeni, bidhaa zilizobaki stoo/eneo la biashara. Watu hawa huhakikisha wanapata taarifa zote muhimu kila siku kabla ya kulala ili kujua hali ya biashara zao. Watu hawa wamefanikiwa kwa kuwa wanayo IMANI, wana KIPAJI na wanayo BIDII katika kazi yao. NMEWAHI KUONA watu wanafanya kazi au biashara na wanapata wateja na kuingiza kipato kikubwa lakini watu hawa hawafanyi maendeleo ya kiuchumi katika maisha yao. Watu hawa ukiwauliza mbona hawafanyi maendeleo watakwambia pesa wakizishika hazikai zinatumika na kuisha bila taarifa, watu hawa siku zote utawaona wanapambana bila kuwepo kwa matokeo chanya katika maisha yao. Hawa ukiwafanyia tathmini utabaini kwamba wana KIPAJI na BIDII lakini hawana IMANI iliyobeba MAARIFA yanayoweza kuwaaminisha kwamba kipato wanachoingiza kinaweza kuleta matokeo makubwa katika maisha yao. Watu hawa wanaishi kwa kukata tamaa wakiamini kwamba kipato wanachokiingiza hakitoshi kamwe kufanya maendeleo. Mwisho kabisa, nikukumbushe ndugu msomaji wa makala zetu, kwamba unaweza kuwa na IMANI, KIPAJI NA BIDII lakini ukanyimwa MAARIFA ambayo yatasababisha wewe kupiga hatua katika kazi au biashara unayoifanya. Kumbuka kwamba MAARIFA unapaswa kuyatafuta yalipo na wakati mwingine unalipa gharama kuyapata, hutaletewa ukiwa umekaa hapo ulipo. Hata fursa za kibiashara hutafutwa na mara nyingi FURSA hutokea bale ambapo JITIHADA zinakutana na BAHATI. Book huduma zetu; 1. Ushauri wa ana kwa ana bila kujumuisha maandalizi ya NYARAKA n.k (120,000/=); 2. Ushauri kupitia simu pekee (40,000/=); 3. Kuandaa NYARAKA ya mpango wa biashara au mradi (150,000 - 500,000/=) 4. Kuzungumza katika tukio (250,000/= bila kujumuisha gharama za kujikimu kama zipo); 5. Kufundisha mada mbalimbali (25,000/=@mshiriki au 250,000/= kwa siku, washiriki wasiozidi 10); Kwa mawasiliano na mialiko yote ya kibiashara piga simu 0672619660 au baruapepe [email protected].