Economist SHILLA Jr.
May 31, 2025 at 12:16 PM
ATHARI ZA CHANGAMOTO BINAFSI ZA KIFEDHA KWA WAFANYAKAZI MAHALI PA KAZI:
Masuala ya kifedha yana uhusiano wa karibu sana na changamoto ya msongo wa mawazo kwa mfanyakazi kwani ndiyo sababu kubwa inayoleta msongo wa mawazo kwa watu wengi. Mara nyingi watu wanakuwa na hofu juu ya uwezo wao wa kifedha hasa kipindi wanapowaza kuhusu marejesho ya mikopo, maandalizi ya kustaafu au kugharamia bili za kila mwezi. Hofu hii inakuwepo hata kwa familia ambazo mume na mke wote wanaingiza kipato, kwa sababu ni ukweli kwamba kipato hakijawahi kutosheleza mahitaji ya kila siku.
Wafanyakazi waliowengi wanapitia changamoto nyingi za kifedha hasa katika eneo la usimamizi wa fedha wanazopata na kufanya maamuzi sahihi ya kifedha. Kwa mujibu wa utafiti uliohusisha mameneja wa rasilimaliwatu 300, asilimia 32 yao walibainisha kwamba matatizo au changamoto binafsi za kifedha kwa wafanyakazi ni changamoto kubwa isiyopewa kipaumbele na waajiri mbalimbali mahali pa kazi.
Changamoto za kifedha kwa wafanyakazi zinasababishwa na wafanyakazi wengi kukosa uelewa, elimu na maarifa ya kifedha ambapo hushindwa kusimamia fedha wanazoingiza na kufanya maamuzi ya kifedha yasiyo sahihi. Maamuzi ya kifedha yasiyo sahihi yanahusisha kukopa mikopo kausha damu yenye riba kubwa, kufanya uwekezaji katika eneo lisilo na faida n.k
Hali hiyo, humletea mfanyakazi msongo wa mawazo mahali pa kazi na kusababisha mfanyakazi kuwa mtoro kazini, kuwa na ufanisi hafifu kazini, kupata maradhi kama shinikizo la moyo, kutokuridhika na malipo ya mwajiri na kutumia muda wa kazi kufanya shughuli binafsi ba kuongeza kipato n.k.
Changamoto za kifedha kwa wafanyakazi hazitatuliwi kwa kuongeza viwango vya mishahara au posho bali Taasisi husika kuwajengea uwezo watumishi wake kwa kutoa mafunzo ya usimamaizi wa fedha na uwekezaji. Baadhi ya Taasisi zina utaratibu wa kutoa mafunzo na semina mbalimbali kuhusu usimamizi wa fedha na uwekezaji, mikopo na madeni, kupanga bajeti na kujiandaa kustaafu. Ingawa kwa waajiri waliowengi jambo hili halifanyiki ama kwa kutokutambua umuhimu wake ama kukosa rasilimali fedha kwa ajili ya kutekeleza jambo hilo. Tunakuachia swali, je mwajiri wako anafanya semina na mafunzo kuhusu usimamizi wa fedha na maandalizi ya kustaafu?
Ukiacha kuwajengea uwezo watumishi, mfanyakazi anaweza kushugulikia changamoto za kifedha kuweka utaratibu wa kuweka akiba, kuwa na bajeti na kuanza kujiandaa kustaafu mapema. Ili kufanikisha haya, mfanyakazi anapaswa kupata uelewa, elimu na maarifa ya kifedha kupitia usomaji wa vitabu mbalimbali, kupitia majukwaa ya mitandao ya kijamii, kupata mtaalam mshauri au kuhudhuria semina na mafunzo mbamlimbali yanayotolewa na kampuni au watu mbalimbali. Maarifa ya kifedha yatamsaidia kufanya maamuzi bora kuhusu masuala ya kifedha na kupunguza msongo wa mawazo.
Book huduma zetu;
1. Ushauri wa ana kwa ana na ufuatiliaji wake bila kujumuisha maandalizi ya nyaraka n.k (Shs. 120,000/=);
2. Ushauri kupitia simu pekee (Shs. 40,000/=);
3. Kuandaa nyaraka ya mpango wa biashara au mradi (Shs. 150,000 - 500,000/=)
4. Kuzungumza katika tukio/semina (Shs. 250,000/= bila kujumuisha gharama za kujikimu kama zipo);
5. Kufundisha mada mbalimbali (Shs. 25,000/=@mshiriki au Shs. 250,000/= kwa siku, washiriki wasiozidi 10);
Kwa mawasiliano na mialiko yote ya kibiashara piga simu 0672619660 au baruapepe [email protected].