Economist SHILLA Jr.
May 31, 2025 at 12:48 PM
MAARIFA NI MAANDISHI NA MAWAZO MAPYA YAPO KATIKA VITABU: UKIJIFUNZA ZAIDI UTAINGIZA PESA ZAIDI; Katika utaratibu wangu wa kila siku wa kusoma vitabu, makala na majarida mbalimbali nilibaini kwamba karibu asilimia 90 ya matajiri duniani ni matajiri wa kizazi cha kwanza. Matajiri hawa utajiri wao sio wa kurithi bali wametengeneza wenyewe. Aidha, tafiti nyingi zinabainisha kwamba karibu matajiri wote hawa wa kizazi cha kwanza walipata mawazo ya biashara na kufanikiwa katika biashara kwa kusoma vitabu na maandiko mbalimbali. Hili linathibitishwa na ukweli kwamba MAWAZO MAPYA HUPATIKANA KATIKA VITABU VYA ZAMANI. Aidha, nilibaini kwamba matajiri hawa kwa mwaka husoma wastani wa vitabu 50, ambapo kwa kwa wiki wanasoma angalau kitabu kimoja. Swali linabaki kwako, unasoma vitabu vingapi kwa siku, kwa wiki, kwa mwezi na kwa mwaka? na Je, utaweza kusoma vitabu 50 kwa mwaka, jaribu na anza sasa, kila kitu kinawezekana hapa duniani. Vilevile, nilibaini kwamba matajiri hawa hawapendelei kusoma vitabu vya Riwaya na Tamthiliya bali husoma vitabu vyenye msaada katika biashara zao wanazofanya. Kwa mfano, matajiri wanasoma zaidi vitabu kuhusu MASOKO, TEKNOLOJIA, USIMAMIZI WA FEDHA, KUWEKA AKIBA, UWEKEZAJI, MAWASILIANO YA KIBIASHARA, USIMAMIZI WA MIRADI n.k. Swali linabaki kwako, unapendelea kusoma vitabu vya aina gani na vyenye maudhui gani? Ukweli ni kwamba maarifa yanayopatikana katika vitabu au maandishi yana msaada mkubwa, kwa sababu, unaweza kuwa na ujuzi fulani, mfano ujuzi wa kufuga kuku, kilimo cha nyanya, n.k sasa jiulize kama huna maarifa kuhusu masoko, uwekezaji, fedha, utawezaje kufanya KILIMO BIASHARA? Ukiweza kupata pesa kupitia maarifa, utabaini kwamba kuna uhusiano katika kujifunza na kuingiza kipato, nikimaanisha kwamba UKIJIFUNZA ZAIDI UTAINGIZA PESA ZAIDI. Dhana hii ni ngumu kueleweka, lakini anza kujifunza leo, uweze kuwa shuhuda wa mabadiliko na mafanikio katika biashara yako au shughuli unayofanya. Kuna faida nyingi za kujifunza zaidi, ikiwemo kuongeza maarifa na uelewa kuhusu jambo fulani, na kukusaidia katika shughuli zako. Aidha, unapo ongeza maarifa unaweza kufanya shughuli zako kwa ufanisi zaidi na kuongeza tija. Vilevile, ukiwa na uelewa wa mambo mengi unaongeza kujiamini ambapo utakuwa na uwezo na utulivu katika kufanya majadiliano ya kibiashara na wakati wa kufanya mawasilisho katika hadhara mbalimbali. Mwisho kabisa narudia Tena MAARIFA YAMEFICHWA KATIKA MAANDISHI NA MAWAZO MAPYA YAMEWEKWA KATIKA VITABU VYA ZAMANI. Kwa hiyo, usichoke kujifunza kila siku, na kwa msaada zaidi usisite kupata ushauri kutoka kwa wataalam washauri. Book huduma zetu; 1. Ushauri wa ana kwa ana na ufuatiliaji wake bila kujumuisha maandalizi ya nyaraka n.k (Shs. 120,000/=); 2. Ushauri kupitia simu pekee (Shs. 40,000/=); 3. Kuandaa nyaraka ya mpango wa biashara au mradi (Shs. 150,000 - 500,000/=) 4. Kuzungumza katika tukio/semina (Shs. 250,000/= bila kujumuisha gharama za kujikimu kama zipo); 5. Kufundisha mada mbalimbali (Shs. 25,000/=@mshiriki au Shs. 250,000/= kwa siku, washiriki wasiozidi 10); Kwa mawasiliano na mialiko yote ya kibiashara piga simu 0672619660 au baruapepe [email protected].

Comments