Economist SHILLA Jr.
June 2, 2025 at 04:23 PM
JENGA TABIA YA KUTAFUTA ELIMU, MAARIFA NA UJUZI, HUKO NDIKO MWANGA WA MAFANIKIO ULIKOJIFICHA: Katika Dunia ya Leo, usijidanganye kufanya maamuzi ya kifedha mfano Uwekezaji bila kuwa na taarifa muhimu katika eneo unalotaka kuwekeza, vinginevyo utakuwa unajipanga kushindwa. Katika Dunia ya Leo, ukiwa na taarifa sahihi na zilizokamilika basi unaweza kufanya maamuzi sahihi kwa karibu asilimia 99.9 na utakuwa na uhakika wa kufanikisha malengo Yako. Katika Dunia ya Leo, wawekezaji wakubwa na wadogo wanawekeza fedha, nguvu na akili zao katika kufanya tafiti za fursa, tafiti za masoko na bei, tafiti za tabia za walaji n.k ili waweze kufanya maamuzi yaliyo sahihi katika uwekezaji wao. Katika Dunia ya Leo, ni wazi na ukweli kwamba katika uwekezaji Kuna vihatarishi vingi na uwezekano mkubwa wa malengo kutokufikiwa kwa sababu mbalimbali kama Hali ya uchumi, mfumuko wa bei, kudorora kwa soko n.k, hivyo kuna umuhimu mkubwa kuwekeza katika kutafuta maarifa, elimu, na ujuzi sambamba na kutafuta taarifa muhimu kupitia tafiti mbalimbali ili uweze kuyafikia malengo yako katika uwekezaji wako. Katika Dunia ya Leo, ukweli ni kwamba unaweza kuwa na elimu Yako katika eneo Fulani, lakini usiwe na maarifa kuhusu biashara, ukakosa maarifa kuhusu masoko na mbinu za majadiliano ya kibiashara na wadau wako n.k, kwa maana hiyo, usiogope kuomba ushauri, kuuliza, kusoma makala mbalimbali, kusoma vitabu, kupitia YouTube na google n.k ili uweze kupata maarifa, elimu na ujuzi unao uhitaji. Katika Dunia ya Leo, unaweza ukasomea ufugaji wa kuku, lakini kumbuka kuwa unahitaji ujuzi, elimu, na maarifa ya kifedha, uwekezaji, masoko, utawala n.k ili uweze kufanikiwa katika biashara Yako. Pamoja na mwelekeo wa Dunia hii, bado hapa kwetu Tanzania, watu hawana utamaduni wa kutafuta ushauri, taarifa, maarifa, ujuzi na elimu katika maeneo wanayotaka kuwekeza au waliyowekeza. Ukweli ni kwamba mafanikio katika uwekezaji au biashara hayana bahati inayotoka pasipojulikana bali ni lazima ufanye uwekezaji wenye tija. Na tija itapatikana kama ukiwekeza kutafuta haya tunayoyaongelea Leo!! Katika Dunia, ya Leo, usiogope kupata ushauri kutoka kwa wataalam ambao wanawekeza muda, akili na fedha kwa ajili ya kuwashauri watu katika maeneo mbalimbali ya utaalam wao. Watu hawa, Wana msaada sana. Usiogope gharama, japo kuna gharama katika ushauri unaopewa kwa kuwa tuna uhakika utaleta matokeo kwako. Mwisho kabisa, katika Dunia ya Leo, hakuna njia ya mkato kuelekekea mafanikio katika shughuli yoyote unayofanya. Kwa hiyo, nasisitiza tena kwamba JENGA TABIA YA KUTAFUTA ELIMU, MAARIFA NA UJUZI, HUKO NDIKO MWANGA WA MAFANIKIO ULIKOJIFICHA. Book huduma zetu; 1. Ushauri wa ana kwa ana bila kujumuisha maandalizi ya NYARAKA n.k (120,000/=); 2. Ushauri kupitia simu pekee (40,000/=); 3. Kuandaa NYARAKA ya mpango wa biashara au mradi (150,000 - 500,000/=) 4. Kuzungumza katika tukio (250,000/= bila kujumuisha gharama za kujikimu kama zipo); 5. Kufundisha mada mbalimbali (25,000/=@mshiriki au 250,000/= kwa siku, washiriki wasiozidi 10); Kwa mawasiliano na mialiko yote ya kibiashara piga simu 0672619660 au baruapepe [email protected].

Comments