Economist SHILLA Jr.
June 4, 2025 at 05:26 AM
MAFANIKIO KATIKA BIASHARA NI IMANI YA MTU ILIYOJIFICHA KATIKA KIPAJI NA BIDII YA KAZI:
NIMEWAHI KUONA wafanya biashara ambao wanauza bidhaa moja kwa zaidi ya miaka 20 na wameweza kujikimu na kufanya maendeleo ya kiuchumi kulingana na kipato wanachoingiza. Wafanyabiashara hawa wanayo IMANI juu ya biashara zao kwamba zinaweza kuwatoa mahali kwenda mahali pengine pa juu zaidi. Wafanyabiashara hawa, huwa hawafikirii kuongeza biashara nyingine wala kupanua au kukuza biashara zao.
Kwa mwenendo huo, utabaini kwamba wafanyabiashara hawa wanayo IMANI kubwa na biashara zao, wana AMINI katika VIPAJI vyao na wamewekeza BIDII katika biashara zao bila kuchoka.
NIMEWAHI KUONA watu wanaofanya biashara kama FAHARI kwa jamii inayowazunguka, na biashara zao zimekuwa zikiwatesa, hawana MUDA wa usimamizi wa biashara, hakuna mgawanyo mzuri wa majukumu katika biashara zao kila mtu ni muuzaji au mhudumu au mhasibu. BIASHARA zinawaletea hasara kila kukicha lakini wanaogopa kufunga biashara kwa sababu wanataka kuiaminisha jamii inayowazunguka kwamba biashara zao zinaenda vizuri na zinawapa faida ili kulinda ufahari wao. Wakati mwingine hutumia kipato chao kingine kuboresha biashara zao kwa kununua bidhaa au malighafi ili biashara zao zisidorore tofauti na utaratibu kibiashara unaosisitiza biashara kujiendesha zenyewe. Watu hawa kwa maneno mafupi ni kwamba IMANI wanayo lakini hawana KIPAJI na BIDII katika kazi.
NIMEWAHI KUONA watu ambao walianza biashara zao na mtaji mdogo katika biashara zao na wameweza kukuza au kupanua bishara zao na kuongeza maeneo ya uwekezaji wao ndani ya kipindi cha miaka mitano (5) hadi 10. Ukiwafuatilia watu hawa wanauwezo mkubwa wa kujenga mahusiano na wateja, wauza malighafi na watu wengine, lakini pia watu hawa wanatumia muda mwingi kuzitafuta fursa za biashara popote zilipo na kuwekeza haraka. Watu hawa wameweka utaratibu mzuri wa usimamizi wa biashara zao, kuanzia ununuzi wa bidhaa, mauzo, ukusanyaji wa mauzo, madeni, bidhaa zilizobaki stoo/eneo la biashara. Watu hawa huhakikisha wanapata taarifa zote muhimu kila siku kabla ya kulala ili kujua hali ya biashara zao. Watu hawa wamefanikiwa kwa kuwa wanayo IMANI, wana KIPAJI na wanayo BIDII katika kazi yao.
NMEWAHI KUONA watu wanafanya kazi au biashara na wanapata wateja na kuingiza kipato kikubwa lakini watu hawa hawafanyi maendeleo ya kiuchumi katika maisha yao. Watu hawa ukiwauliza mbona hawafanyi maendeleo watakwambia pesa wakizishika hazikai zinatumika na kuisha bila taarifa, watu hawa siku zote utawaona wanapambana bila kuwepo kwa matokeo chanya katika maisha yao. Hawa ukiwafanyia tathmini utabaini kwamba wana KIPAJI na BIDII lakini hawana IMANI iliyobeba MAARIFA yanayoweza kuwaaminisha kwamba kipato wanachoingiza kinaweza kuleta matokeo makubwa katika maisha yao. Watu hawa wanaishi kwa kukata tamaa wakiamini kwamba kipato wanachokiingiza hakitoshi kamwe kufanya maendeleo.
Mwisho kabisa, nikukumbushe ndugu msomaji wa makala zetu, kwamba unaweza kuwa na IMANI, KIPAJI NA BIDII lakini ukanyimwa MAARIFA ambayo yatasababisha wewe kupiga hatua katika kazi au biashara unayoifanya. Kumbuka kwamba MAARIFA unapaswa kuyatafuta yalipo na wakati mwingine unalipa gharama kuyapata, hutaletewa ukiwa umekaa hapo ulipo. Hata fursa za kibiashara hutafutwa na mara nyingi FURSA hutokea bale ambapo JITIHADA zinakutana na BAHATI.
Book huduma zetu;
1. Ushauri wa ana kwa ana bila kujumuisha maandalizi ya NYARAKA n.k (120,000/=);
2. Ushauri kupitia simu pekee (40,000/=);
3. Kuandaa NYARAKA ya mpango wa biashara au mradi (150,000 - 500,000/=)
4. Kuzungumza katika tukio (250,000/= bila kujumuisha gharama za kujikimu kama zipo);
5. Kufundisha mada mbalimbali (25,000/=@mshiriki au 250,000/= kwa siku, washiriki wasiozidi 10);
Kwa mawasiliano na mialiko yote ya kibiashara piga simu 0672619660 au baruapepe [email protected].