Economist SHILLA Jr.
June 7, 2025 at 05:30 AM
KATIKA MAISHA, KILA MTU ANA CHANGAMOTO ZAKE, JITAHIDI KUITAFUTA FURAHA YA KWELI: Mtu unayemdhania kuwa anayo FURAHA maishani mwake ukipata fursa ya kuingia moyoni mwake utabaini kwamba ana magumu mengi anayopambana nayo kila siku. Na hayo magumu yanaweza kuwa zaidi ya yale yanayokusibu wewe. FAMILIA unayodhania kuwa inayo furaha kila siku, wakati mwingine usiombe kuingia ndani yake kwa sababu utakuta wanazi changamoto nyingi ambazo ni nafuu kuliko changamoto zako na familia yako. FURAHA katika maisha haipimwi kwa kutazama kwa macho au kuangalia vitu anavyomiliki mtu, wala furaha haiwakilishi UTAJIRI AU UMASKINI mtu au familia bali ni inapimwa kwa mazingira ya maisha, matukio katika maisha, mahusiano katika maisha na mchakato/njia za utafutaji wako hadi kufikia mafanikio au utajiri au hali uliyonayo sasa. Usichukulie poa, mchakato unaopitia katika utafutaji wako, unaweza kuwa ndiyo chanzo cha wewe kuwa na furaha au kukosa furaha. Katika mazingira ya maisha ya kila siku unaweza kukutana na TAJIRI anyeishi maisha ya KITAJIRI kufurahisha UMMA lakini ndani yake hana FURAHA na ukamkuta MASKINI anaishi maisha ya kawaida ya KIMASKINI lakini anayo FURAHA yeye na familia yake. Jitathmini wewe na familia yako kama mnaishi maisha ya furaha na kitu Gani kinaleta hiyo furaha?? Ninakushauri leo, kufanya uchunguzi wa kina wa maisha yako hasa michakato ya maisha yako katika utafutaji wako au aina maisha yako kama inaleta furaha au huzuni katika maisha yako. Nakukumbusha kwamba Utajiri au umasikini siyo chanzo Cha furaha maishani, CHUNGUZA maisha yako na UITAFUTE FURAHA YA KWELI! KAMA KUNA JAMBO UMEJIFUNZA TUAMBIE KWENYE COMMENT NA USIACHE KUSAMBAZA (SHARE) ANDIKO HILI. Book huduma zetu; 1. Ushauri wa ana kwa ana bila kujumuisha maandalizi ya NYARAKA n.k (120,000/=); 2. Ushauri kupitia simu pekee (40,000/=); 3. Kuandaa NYARAKA ya mpango wa biashara au mradi (150,000 - 500,000/=) 4. Kuzungumza katika tukio (250,000/= bila kujumuisha gharama za kujikimu kama zipo); 5. Kufundisha mada mbalimbali (25,000/=@mshiriki au 250,000/= kwa siku, washiriki wasiozidi 10); Kwa mawasiliano na mialiko yote ya kibiashara piga simu 0672619660 au baruapepe [email protected].

Comments