Legal Minds Forum ⚖️
June 8, 2025 at 07:57 AM
Majibu ya swali la Pili.
Jibu ni HAPANA.
Hapana, katika Mahakama za Mwanzo nchini Tanzania, maombi hayawezi kuwasilishwa kwa njia ya chamber summons inayoungwa mkono na affidavit kama inavyofanyika katika Mahakama za Wilaya, Mahakama ya Hakimu Mkazi, au Mahakama Kuu. Badala yake, taratibu maalum zimewekwa kwa mujibu wa Sheria ya Mahakama za Mahakimu (The Magistrates' Courts Act) na Kanuni zake.
Taratibu za Maombi katika Mahakama za Mwanzo:
1. Maombi ya Mdomo au Maandishi: Kwa mujibu wa Kanuni ya 5 ya The Magistrates’ Courts (Civil Procedure in Primary Courts) Rules maombi yanaweza kufanywa kwa mdomo au kwa maandishi. Ikiwa maombi yanafanywa kwa mdomo, maelezo yake yanapaswa kurekodiwa na hakimu au mahakama.
2. Fomu Maalum: Maombi yanapaswa kutumia fomu zilizoidhinishwa na Jaji Mkuu, kulingana na Kanuni ya 4 ya kanuni hizo. Hii inamaanisha kuwa kuna fomu maalum zilizotolewa kwa ajili ya matumizi ya Mahakama za Mwanzo.
3. Maombi ya Mdomo:Kwa maombi ya mdomo, hakimu anapaswa kurekodi kiini cha maombi hayo katika kumbukumbu rasmi za mahakama.
THEREFORE
Katika Mahakama za Mwanzo, maombi hayawezi kuwasilishwa kwa njia ya chamber summons inayoungwa mkono na affidavit. Badala yake, maombi yanaweza kufanywa kwa mdomo au kwa maandishi, kwa kutumia fomu maalum zilizoidhinishwa na Jaji Mkuu, na kufuata taratibu zilizowekwa katika The Magistrates’ Courts (Civil Procedure in Primary Courts) Rules
👍
2