
Legal Minds Forum ⚖️
1.1K subscribers
About Legal Minds Forum ⚖️
Justice must not only be done but must be seen to be done
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

Mahakama ya Rufaa ya Tanzania leo imetoa uamuzi katika kesi ya kikatiba ya Rufaa Na. 134 ya Mwaka 2022, iliyofunguliwa na mtetezi wa haki za binadamu, Wakili Onesmo Olengurumwa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Rufaa hiyo ilisikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa: Jaji Rehema Levira, Jaji Wilfred Rumanyika na Jaji Gerald Ngwembe. Wakili Olengurumwa aliwakilishwa na jopo la mawakili maarufu likiongozwa na Prof. Issa Shivji pamoja na Dkt. Rugemeleza Nshala, Mpale Mpoki na Wakili John Seka. Kesi hiyo ilihusu kupinga vifungu vya Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) ya mwaka 2020, vilivyobadili Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi na Wajibu (Sura ya 3) kwa kuongeza vifungu vya 4(2), 4(3), 4(4), na 4(5). Vifungu hivyo vilionekana kuweka vikwazo katika mashauri ya kikatiba yenye maslahi kwa umma, maarufu kama Public Interest Litigation. Maelezo ya Vifungu Vilivyolalamikiwa: Kifungu cha 4(2): Kilihitaji mtu anayetaka kufungua kesi ya kikatiba kuambatanisha kiapo kinachoeleza namna alivyoathirika binafsi na ukiukwaji huo. Kifungu cha 4(3): Kiliongeza kizuizi kwa mashauri ya maslahi ya umma kwa kutaka mlalamikaji aonyeshe maslahi binafsi sawa na Ibara ya 30(3) ya Katiba. Kifungu cha 4(4): Kiliweka sharti kuwa kesi dhidi ya viongozi waandamizi serikalini – Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika, Naibu Spika na Jaji Mkuu – zifunguliwe dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali badala ya wahusika hao moja kwa moja. Kifungu cha 4(5): Kilimtaka mtu anayepanga kufungua kesi kutafuta kwanza nafuu kupitia sheria nyingine zilizopo kabla ya kufungua kesi chini ya Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi. Awali, Mahakama Kuu ya Tanzania iliitupilia mbali kesi hiyo mnamo Februari 15, 2022, kwa maelezo kuwa vifungu hivyo havivunji Katiba wala mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu. Mahakama Kuu ilisisitiza kuwa vifungu hivyo vinakamilisha Ibara ya 26(2) na 30(3) ya Katiba, na vinaakisi misingi ya utawala wa sheria, mgawanyo wa madaraka, na mfumo wa kimataifa wa haki. Hata hivyo, Wakili Olengurumwa hakuridhika na uamuzi huo na kukata rufaa Mahakama ya Rufaa mwaka huo huo wa 2022. Uamuzi wa Mahakama ya Rufaa Leo Juni 13, 2025, Mahakama ya Rufaa kupitia kwa Naibu Msajili Mhe. Joseph Fovo, imesoma uamuzi huo kwa njia ya mtandao na kubatilisha vifungu vyote vinne vilivyolalamikiwa. Kwa mujibu wa Mahakama ya Rufaa: Kifungu cha 4(2) kinavunja dhana ya mashauri ya maslahi kwa umma kwa kuhitaji waathirika binafsi pekee, hali inayokinzana na Ibara ya 26(2) ya Katiba. Kifungu cha 4(3) ni batili kwa kuwa kinachanganya masharti ya Ibara ya 30(3) (maslahi binafsi) na haki za maslahi kwa umma zinazolindwa chini ya Ibara ya 26(2). Kifungu cha 4(4) ni batili kwa kuwa Mwanasheria Mkuu hana mamlaka ya kikatiba kuwakilisha mihimili mingine, hasa Mahakama au viongozi wa kisiasa walio huru kikatiba kama Jaji Mkuu. Kifungu cha 4(5) pia ni batili kwa kuwa hakuna sheria nyingine zinazotoa nafuu ya moja kwa moja kwa mashauri ya maslahi ya umma. Agizo kwa Bunge Mahakama ya Rufaa imeagiza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuta vifungu hivyo vinne ndani ya kipindi cha miezi 12 kuanzia tarehe ya hukumu. Uamuzi huu umetajwa kuwa ushindi mkubwa kwa wanaharakati wa haki za binadamu na wananchi wanaotetea masuala ya kijamii kupitia Mahakama.

_Hearing is not considered unfair if individuals choose not to exercise their rights during an administrative process. The requirements of fairness are met if people are given a genuine opportunity to understand the case against them and present their own case. They should not be compelled to attend hearings, make submissions, or utilize procedural rights if they don't wish to._


Nani anatakiwa kusaini pleadings (nyaraka) za kwenda Mahakamani kwenye kesi ya madai? ⏬⏬⏬⏬

The best Constitutional Case(Judgment) ya Mwaka huu. Make sure you read it! You'll learn a lot. 0744730742 +255 623 759 800 #LegalMindsForum #Ijuesheria #FanyaKazi


Nyaraka za kufungulia na kujibu kesi Mahakamani (Pleadings) kama vile hati ya madai (plaint) na hati ya utetezi (WSD) zinatakiwa kusainiwa na mhusika (mdai au mdaiwa) pamoja na wakili wake (kama yupo) au mtu yeyote ambaye ameruhusiwa na mhusika. Hata wakili peke yake anaweza kusaini kama tu ameruhusiwa na mteja wake. Hii ni kwa mujibu wa kifungu au Order VI(14) ya Sheria ya Mwenendo wa kesi za madai (Civil Procedure Code au kwa kifupi tunaiita 'CPC'). Tazama pia maamuzi ya Mahakama ya Rufani kwenye Kesi ya AGATHA MSHOTE Vs EDSON EMMANUEL, CIVIL APPEAL NO. 121 OF 2019. Kama nyaraka isiposainiwa kabisa na mhusika ni kosa kisheria au ikisainiwa na mtu mwingine ambaye hana mamlaka au hajaruhusiwa ni kosa kisheria, na inaweza kupelekea kesi yako kufutwa kwa sababu ya kutumia nyaraka mbovu (defective plaint or WSD).


Update kutoka kwa _MENDEZ_ *KESI YA KANISA LA GWAJIMA: Serikali inasema haijafuta* Kanisa la Gwajima - *hakuna maamuzi ya kufuta* Kanisa la Gwajima linaloenda kwa *jina la Glory of Christ TANZANIA Church*. Na wala *Barua ya kufuta haijawahi kupelekwa kwenye Kanisa hilo.* Kwamba, *kinachoonekana kufutwa kwenye ile Barua* ya Msajili wa Jumuiya, *ni Kanisa linaloitwa Glory of Christ Church* (hakuna neno *TANZANIA*). 👆🏿 Kwahiyo, kwasababu *aliyeleta Maombi* ya Zuio na kutaka hali irudi kama ilivyokuwa _(status quo ante)_ *ni Glory of Christ TANZANIA Church* ambaye hakuna maamuzi ya kumfuta, *Serikali imeweka pingamizi* kwamba *Mahakama haina* mamlaka ya kusikiliza maombi hayo. Kama ni hivyo👆🏿, *kwanini sasa Polisi walienda kwenye kanisa la Glory of Christ TANZANIA Church* kuzuia shughuli zisiendelee na kuwakamata Waumini *wakidai wanatekeleza Amri ya Msajili kulifunga kanisa hilo?* Ni hoja ya upande wa pili wakipinga pingamizi na kusema hiyo imewafanya wakate Rufaa kwa Waziri na kuleta maombi haya Mahakamani. Mahakama Kuu imesema *haioni ni kwa namna gani Mamlaka yake yameporwa. Imetupilia mbali pingamizi.✍🏼* _MD, Mendez (M.C.A)_ 09/06/2025

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Mei 19, 2025 imeahirisha Kesi ya Uhaini inayomkabili Wakili Tundu Lissu, mpaka Juni 2, 2025.


_Damian Ruhele v. Republic, Criminal Appeal No. 501 of 2007 (unreported). _ When you fail to cross-examine a witness on asserted facts, the trier of fact (judge or jury) may assume those facts to be accurate, as they haven't been challenged. This is because cross-examination allows for the questioning of witness credibility and the potential exposure of weaknesses in their testimony, which helps the trier of fact assess the truthfulness of the evidence. Without cross-examination, the evidence is presented without a proper challenge, potentially leading to an inaccurate conclusion.
