Chama Imara Na Samia

Chama Imara Na Samia

205.5K subscribers

Verified Channel
Chama Imara Na Samia
Chama Imara Na Samia
May 19, 2025 at 04:42 PM
GAVU AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KUTEMBELEA MAKAO MAKUU YA HISENSE KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Idara ya Oganaizesheni, Ndg. Issa Gavu ameuongoza ujumbe wa Tanzania uliopo China, kutembelea makao makuu ya Kampuni ya uzalishaji vifaa vya kielektroniki ya Hisense yaliyopo katika mji wa Qindao, nchini humo. Gavu na ujumbe wake huo kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamefanya ziara hiyo kiwandani hapo ikiwa moja ya shughuli zilizopo katika ratiba ya ziara hiyo. ziara hiyo ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania na China, pamoja na kudumisha uhusiano kati ya CCM na Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC). == ==

Comments