WATANI WA JADI
WATANI WA JADI
May 18, 2025 at 09:36 AM
RS BERKANE WENYEWE WAMEONA WAMEFELI LAKINI WAPINZANI WA SIMBA SC WAMEFURAHI NA KUHISI SIMBA AMEPOTEZA FAINALI. Niaze kwa kuwasalimu kwa salamu ya club ya simba sc (simba nguvu moja) nikirudi kwenye chambuzi zangu kwa jicho pevu sana juu na nini nilicho kiona kwenye mechi hii kilicho igharimu simba kwenye mechi ya first leg hakuna isipokuwa homa ya fainali yenyewe.. Rs Berkane waliwasoma vyema Simba sc na kufanyia kazi vyema ubora na udhaifu wa simba... Simba ni club ambayo inacheza soka la kisasa na ina bench la ufundi ambalo linaamini juu ya mbinu bora za kisasa za soka duniani.. tunapo zungumza soka la kisasa tunamaanisha mfumo wa (BUILD UP) Hii ni aina ya mpira ambao timu husika huanza kuanzia kwa goalkeeper na kucheza na mabeki wake na kuanza kujenga mashambulizi kuanzia nyuma, kipa hana ruhusa ya kupiga mpira mbele akianza goal kick bali huanza kwa full back zake au center back wake na taratibu transmission huanzia nyuma na kuhamia eneo la kati na kusogea kwenye eneo la mpizani kwa possession au pasi nyingi.. huu ndio mpira wa kisasa wa build up play unavyo fanya kazi.. ni mfumo bora sana wa kujilinda kwasababu unamnyima adui mpira muda mrefu na kubakia kwako lakini ni mfumo hatari sana sawa na kidonge cha sumu lakini chenye kutibu maradhi sugu.. unapokosea masharti yake basi huwa sumu na kukudhuru haraka.. Kwanini nasema Rs Berkane waliifanyia kazi sana mechi hii kwa kuwasoma sana simba sc ni kuwa waligunduwa mfumo mama wa Fadlu Devis kuwa anatumia Build Up football system na wao wakaja na mfumo wa HIGH DEFENSEIVE LINE system ambayo ndio master key🔑 ya mfumo wa Build up system.... Rs Berkane wali press kwa takriban dakika 20 za kipindi cha kwanza kuhakikisha wanailazimisha simba kufanya makosa mengi kwenye eneo lao na kufanikisha matokeo na ndio style ya uchezaji ya RS Berkane wanapocheza na mfumo wao wa HIGH DEFENSEIVE LINE. Mpira wa kona ulio mkuta Kamara kiungo wa ulinzi wa Berkane na kupiga kichwa na kuandika bao la kwanza ni matokeo ya pressing waliyopelekewa simba dakika za awali na pia mpira alio nyang'anywa Kagoma akipokea pasi butu kutoka kwa Pin pin Kamara ni matokeo ya pressing ya Berkane ndani ya dakika za mwanzo pamoja na kuwa kulikuwa na viashiria vya foul wakati wa unyanganyaji huo ulifanyika na muamuzi alishindwa kuona kutokana na presha ya mchezo.. Wakati wa dakika 30 za mwanzo za mchezo ilionesha wazi kuwa RS Berkane wangeimaliza fainali hii pale kwao lakini taratibu mambo yalianza kubadilika na simba kurudi mchezoni na kuanza kuhimili presha ya mchezo huku ubao ukisoma 2-0 kitu ambacho hakikuwa mpango wa Berkane kutokana na ukweli kuwa wapinzani wao Simba sc wana historia nzuri sana kwenye mechi za nyumbani kwenye mechi za mkakati kama hizi.. ushindi wa goli mbili bado unaifanya mechi ya second leg kuwa wazi kutokana na aina ya mpizani wa Berkane anapokuwa Benjamin mkapa stadium. Simba Sc wameonja presha ya Berkane na wamei feel vyema na sasa kurudi kwa mkakati wa kuhakikisha wanasawazisha magoli mawili ndani ya kipindi cha kwanza Benjamin Mkapa Stadium na kipindi cha pili ni kutafuta ushindi na kulinakisha kombe hili Tanzania.. Inawezekana na uwezo huo simba wanao wakipunguza makosa na kusimama imara kimaamuzi uwanjani.. Mungu ibariki Simba sc Nguvu moja.....
Image from WATANI WA JADI: RS BERKANE WENYEWE WAMEONA WAMEFELI LAKINI WAPINZANI WA SIMBA SC WAMEF...

Comments