
WATANI WA JADI
65 subscribers
About WATANI WA JADI
*Chambuzi mbalimbali za soka la Tanzania Afrika na Duniani kote utazipata hapa kwa uhakika zaidi* Kwa matangazo ya biashara michezo ya aina yoyote pia utaipata hapa
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

Jamani tuwe tunalike au dislike support ni ndogo sana au hizo hamzihitaji tubadili agenda za kuleta humu?

MICHEZO 🚨 JEMEDARI AWACHANA YANGA ACHENI UONGO HAKUNA PESA MNADAI HESABU ZENU SI SAHIHI ANAANDIKA JEMEDARI..... 👇 Yanga SC wanasema wao ndiyo wanaidai TFF 226M baada ya kutoa makato yao mengine yote. Yani kabla ya kwenda kuonana na idara ya Fedha ya TFF hapo kesho wameamua kutoa tahadhari kwamba wao ndio WADAI na Sl WADAIWA. BAHATI MBAYA SANA kwenye hizo hesabu hapo Yanga SC wamesema Ubingwa wa CRDB Confederation Cup msimu wa 2023/2024 ni 200M kitu ambacho SI KWELI. Ubingwa wa Kombe la Shirikisho ni 50M miaka yote haijawahi kubadilika hata siku moja, manake kwenye hizo hesabu zao kuna nyongeza ya 150M ambayo ni MAKOSA. Hivyo basi 226M ukitoa 150M unabakiwa na 76M. Mwaka jana tarehe 7 Agosti walituma TFF barua yenye Kumb:Na YAHLYSC/TFF/2024/330 ikiwa na kichwa cha Habari YAH: VIBALI KWA WAGENI. Ambapo katika barua hiyo wanasema kutokana na kupanda kwa gharama za wachezaji wa kigeni kutoka 4M hadi 8M kwa mchezaji 1, wanaomba kuongeza kiasi cha 48M ambacho wanapenda kikatwe kutoka kwenye pesa zao za zawadi, Kiasi cha 48M HAKIJAWEKWA hapo kwenye jedwali/barua iwe kwa makusudi au bahati mbaya. 76M ukitoa 48M unabakiwa na 28M, lakini Yanga SC kama vile haitoshi tarehe 5 February 2025 waliandika barua yenye Kumb Na: YAH.YSC/TFF/2025/019 yenye kichwa cha habari YAH: UTAMBULISHO WA MAKOCHA WAPYA. Ambapo waliwatambulisha makocha Miloud Hamd na Nassim Anisse na kuomba ada ya malipo kiasi cha dola za Marekani 450 (Tshs 1.2M) zikatwe kutoka kwenye pesa zao za Ushindi zilizopo TFF Hapo ina maana kwenye 28M inabaki 27M. Kama Yanga SC huo ndio mwenendo wao wa kupokea pesa kidogo kidogo na baadae kuonyesha WAMESAHAAU basi huenda kesho kikao na TFF kikawa KIFUPI MNO manake watapewa nyaraka zao tu. NB: Nimeuona mchanganuo wa madeni na malipo ambayo Yanga SC wamelipwa, kama wakikubali hivyo ndivyo ilivyokuwa basi narudia kusema kikao kitakuwa KIFUPI MNO guys.

Mnaionaje ligi ya Tanzania kutokana na sakata hili tutabaki salama kama ligi?


Utopolo alikuwa na ball possesion 88 na alikuwa anaongoza 1 ghafla CRDB akaingilia mechi na kuwafanya utopolo kupata magoli 2 ya haraka na wakawa wanaongoza 3 ila ghafla TFF nao wamefanya bonge la comeback Dakika ya 70 TFF 5 utopolo 3 Ninavyowajua mimi hawa ndugu zetu walivyokuwa hawawezi kuwa wavumilivu basi tutegemee TAARIFA YA UMMA muda wowote kuanzia sasa 😂😂😂😂


Haya maagizo yaliyotolewa june 5 hatimaye jana june 13 yametekelezwa je nani mbabe 🤝...Maagizo ni kwamba Kiongozi yoyote atakaepeleka timu Uwanjan Juni 15 basi atafute na timu nyingine {yaan aachie ngazi ya Uongozi kwenye Klabu yetu ✊)


HAYAWI HAYAWI YAMEKUWA HUKO KWENU Awamu hii mnatoka vipi? 🤣🤣🤣🤣 ‼️ KWA HESHIMA ‼️ Kuna kajiupendeleo flani ambacho sio Sawa kiukweli Kipindi kile utopolo wanaingia fainali ya kombe la shirikisho walipopewa medali walipewa heshima ya kukaribishwa ikulu na kupewa pongezi kwa walichokifanya ila imekuwa tofauti kwa SIMBA yetu tumetelekezwa kama watoto yatima💔💔💔 Na hata Leo nilipoona zile sura za viongozi wetu baada ya kutoka kuonana na mama nilihisi tu kuna vitu haviko sawa kabisa , kuna nyakati mtu anaweza kushinikizwa akubali maamuzi ambayo hajaridhika nayo kwa kuheshimu mamlaka ila hii sio sawa Kanuni gani imetumika kuvunja mechi ya tarehe 15 ??? Kama akuna sababu ya wenzetu ilivunjwa na wenzetu wakaja na masharti na yote yanaenda kutekelezwa ndo maana wamekubali kucheza vipi kuhusu sisi ???? Viongozi wetu mukikubali kucheza mechi ya tarehe 25 kumbukeni kuna kupoteza pia itakuwa ngumu mnooo watu kukueleweni, Huu unyonge hapana kiukweli lazima vitu vingine tuvipinge kwa maslahi ya SIMBA yet sio kila kitu ndio mzee alafu sisi tunaumia. .. ✍🏽 Ommy Simba Sauti Ya Msimbazi ✅

Yanga anaidai TFF millioni mia nne laki nne na elfu tisini je watailipa au wajiuzulu 😂😂😂😂 Kazini kwangu kunakazi


Dah hii ndio bongo wakati Yanga wanatoa shinikizo miamba inaendelea kujiengua hadi huruma 😂😂😂😂🙌🙌🙌🙌
