
NMB Bank Plc
May 24, 2025 at 06:46 PM
Mafinga, Iringa 📍
Hata wewe si unaona walivyo-enjoy!
Tunaendelea na programu yetu ya Nondo za Pesa, ambayo ni mkakati maalum wa kufikisha elimu ya fedha kwa watanzania wengi zaidi, hasa maeneo ambayo bado hayajafikiwa. Lengo ni kuwawezesha kufikia malengo yao kupitia masuluhisho yetu ikiwemo bima, mikopo, na huduma za kidijitali.
Mbali na elimu ya kifedha, tumetoa pia Elimu ya Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia, semina kwa vyama na vikundi vya kijamii, kukabidhi na kupanda miti zaidi ya 600 na bonanza lililo sheheni burudani mbalimbali!
Tukio hili lilifanyika Kwenye kijiji cha Igowole, Mafinga na uwakilishi wa Benki umeongozwa na Meneja wetu wa Mauzo wa Kanda ya Nyanda za Juu, Manyilizu Masanja kwa niaba ya Meneja wa Kanda.
#nmbkijijiday
#nmbkaribuyako

👍
❤️
😂
🙏
7