
NMB Bank Plc
June 10, 2025 at 07:58 AM
Tumeshiriki katika Maadhimisho ya Miaka 10 ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu 2025, yaliyofunguliwa rasmi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Alexander Mkumbo katika Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kuanzia tarehe 9 hadi 11 Juni, 2025.
Maonesho haya yenye kaulimbiu “Kuvuna Fursa za Teknolojia ya Kidijitali Kuongeza Kasi ya Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Biashara,” yanalenga kuhimiza ushirikiano kati ya sekta ya elimu, biashara, na teknolojia katika kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Benki ya NMB imeshiriki kama mdhamini na mshiriki hai kwa lengo la kuendeleza juhudi zake katika kukuza elimu, teknolojia na ubunifu kwa kila Mtanzania kupitia huduma zake za kidijitali.
Uwakilishi wa Benki ya NMB umeongozwa na Meneja Mwandamizi kutoka Idara ya Ubunifu, Bi. Jacqueline Nnunduma aliyeambatana na wafanyakazi wengine wa Benki.
#nmbkaribuyako

❤️
1