
NMB Bank Plc
June 10, 2025 at 01:55 PM
Tunaendelea kuandika historia!
Kupitia azma yetu ya kuhakikisha tunaleta tija na faida kubwa kwa wawekezaji wetu, leo tumekabidhi gawio la Tsh. Bilioni 68.1 kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye umiliki wa 31.8% katika Benki yetu. Hili ni ongezeko la 19% kutoka gawio la Tsh Bilioni 57.4 mwaka jana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyeambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, wamepokea mfano wa hundi kutoka kwa Mwenyekiti wetu wa Bodi ya Wakurugenzi - David Nchimbi pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wetu – Bi. Ruth Zaipuna katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Pia, Benki imepokea tuzo ya kutambua mchango wetu katika kutoa gawio kubwa kwa Serikali, mwaka hadi mwaka.
Tunawashukuru wadau wetu wote kwa kuendelea kutuamini na kuwa sehemu ya mafanikio haya.
#nmbkaribuyako

❤️
👍
🙏
5