
Tanzania Institute of Accountancy (TIA)
May 15, 2025 at 05:42 PM
TIA NA BRELA WAMEUNGANISHA NGUVU KUWAJENGA VIJANA KITAALUMA
Wanafunzi zaidi ya 200 kutoka TIA wameshiriki warsha ya Uendeshaji na Usimamizi wa Biashara iliyoandaliwa kwa ushirikiano na BRELA kupitia Mpango wa Maendeleo ya Taaluma.
Warsha hii imewapatia maarifa ya usajili wa kampuni, majina ya biashara, haki miliki na leseni za biashara ili kuwawezesha kuanzisha na kuendesha biashara kwa mafanikio.
Ushirikiano kati ya TIA na BRELA umedhamiria kuwajengea uwezo vijana na wajasiriamali chipukizi ili kufanikisha malengo yao ya kibiashara na kuchochea maendeleo ya uchumi wa taifa.
#tiatanzania
#brela
#ujasiriamali
#maendeleoyataaluma
#biasharatanzania
#tiaelimukwaufanisi
#tiatanzaniaupdates
👍
3