
Tanzania Institute of Accountancy (TIA)
14.8K subscribers
Verified ChannelAbout Tanzania Institute of Accountancy (TIA)
Ukurasa rasmi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

UBALOZI WA URUSI WATEMBELEA TIA KWA USHIRIKIANO WA KITAMADUNI Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Dar es Salaam, imepokea ugeni kutoka Ubalozi wa Urusi ukiongozwa na wahariri wa mashairi Andrey Polonsky na Igor Karaulov, kwa lengo la kuimarisha mabadilishano ya kitamaduni. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Dkt. Momole Kasambala, amesema ushirikiano huo utachangia kukuza maarifa ya kimataifa kwa wanafunzi na wahadhiri kupitia elimu na ubunifu. Wageni hao walishiriki mijadala ya fasihi na utamaduni wa Urusi pamoja na wanafunzi, wakieleza historia na maadili ya kifasihi ya nchi yao. Vilevile, Ubalozi wa Urusi ulikabidhi vitabu vya hadithi kwa uongozi wa TIA kama mchango wa kuimarisha ushirikiano wa kielimu kati ya mataifa hayo mawili. #tiaelimukwaufanisi #tiatanzania #tiatanzaniaupdates


TIA NA BRELA WAMEUNGANISHA NGUVU KUWAJENGA VIJANA KITAALUMA Wanafunzi zaidi ya 200 kutoka TIA wameshiriki warsha ya Uendeshaji na Usimamizi wa Biashara iliyoandaliwa kwa ushirikiano na BRELA kupitia Mpango wa Maendeleo ya Taaluma. Warsha hii imewapatia maarifa ya usajili wa kampuni, majina ya biashara, haki miliki na leseni za biashara ili kuwawezesha kuanzisha na kuendesha biashara kwa mafanikio. Ushirikiano kati ya TIA na BRELA umedhamiria kuwajengea uwezo vijana na wajasiriamali chipukizi ili kufanikisha malengo yao ya kibiashara na kuchochea maendeleo ya uchumi wa taifa. #tiatanzania #BRELA #Ujasiriamali #MaendeleoYaTaaluma #BiasharaTanzania #tiaelimukwaufanisi #tiatanzaniaupdates