Tanzania Institute of Accountancy (TIA)
Tanzania Institute of Accountancy (TIA)
May 26, 2025 at 10:13 AM
UBALOZI WA URUSI WATEMBELEA TIA KWA USHIRIKIANO WA KITAMADUNI 
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Dar es Salaam, imepokea ugeni kutoka Ubalozi wa Urusi ukiongozwa na wahariri wa mashairi Andrey Polonsky na Igor Karaulov, kwa lengo la kuimarisha mabadilishano ya kitamaduni. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Dkt. Momole Kasambala, amesema ushirikiano huo utachangia kukuza maarifa ya kimataifa kwa wanafunzi na wahadhiri kupitia elimu na ubunifu. Wageni hao walishiriki mijadala ya fasihi na utamaduni wa Urusi pamoja na wanafunzi, wakieleza historia na maadili ya kifasihi ya nchi yao. Vilevile, Ubalozi wa Urusi ulikabidhi vitabu vya hadithi kwa uongozi wa TIA kama mchango wa kuimarisha ushirikiano wa kielimu kati ya mataifa hayo mawili. #tiaelimukwaufanisi #tiatanzania #tiatanzaniaupdates
Image from Tanzania Institute of Accountancy (TIA): UBALOZI WA URUSI WATEMBELEA TIA KWA USHIRIKIANO WA KITAMADUNI 
Taasisi...
❤️ 😢 4

Comments