Tanzania Institute of Accountancy (TIA)
Tanzania Institute of Accountancy (TIA)
May 27, 2025 at 09:50 AM
TIA YAWAKUTANISHA WANAFUNZI NA FURSA ZA MASOMO MAREKANI 
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), kampasi ya Dar es Salaam, iliandaa warsha kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani kwa lengo la kuwapa wanafunzi taarifa kuhusu fursa za elimu ya juu nchini Marekani. Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Prof. William Pallangyo, aliwapokea na kuwashukuru wageni hao kwa kushirikiana na taasisi yake kuwafikia wanafunzi na wafanyakazi wa TIA. Warsha hiyo ilifunguliwa na Dkt. Momole Kasambala, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, ambaye alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika kuwawezesha vijana kielimu na kiuchumi. Wageni kutoka Ubalozi wa Marekani waliongozwa na Bwana Chad Morris, aliyetoa mwongozo wa kuomba masomo na fursa zilizopo kwa wanafunzi wa kimataifa, huku Bi Tracy Milyango akihimiza maandalizi ya mapema na matumizi ya programu ya EducationUSA. Warsha hiyo ilihudhuriwa na wanafunzi na wafanyakazi waliopata nafasi ya kuuliza maswali kuhusu masomo, ufadhili na vigezo vya kujiunga na vyuo vya Marekani. #tiaelimukwaufanisi #tiatanzania #tiatanzaniaupdates
❤️ 👍 4

Comments