๐ข๐ง๐๐จ๐ ๐๐ก ๐๐๐๐ง
May 23, 2025 at 02:15 PM
Watu wengi wanaingia kwenye mahusiano wakiamini wanapendwa, kumbe wanahitajika tu. Kupendwa na kuhitajika ni maneno mawili ambayo mara nyingi huchanganywa, lakini kiuhalisia yana tofauti kubwa sana.
Kupendwa ni mtu kukujali kwa dhati, kukuona wa thamani bila kuangalia faida yoyote anayopata kutoka kwako.
Atakuheshimu hata mbele za watu. Atakuelewa hata katika mapungufu yako. Atachagua kukusamehe, hakukuacha. Atakutafuta hata ukiwa huna chochote cha kutoa.
Tafiti za kisaikolojia zinaonyesha kuwa watu wanaohisi kupendwa kwa dhati hupata viwango vya juu vya utulivu wa kihisia na afya ya akili.
Kuhitajika kunakuwa ni kwa sababu unatoa msaada, faraja, pesa, au hata kuondoa upweke kwa mtu (ngono). Wakati mwingine mtu anakuambia โnakupendaโ kumbe maana yake ni: โNakuhitaji kwa sasa.โ
Mtu anayekuhitaji:
Anaweza kukuacha akipata mtu mwingine mwenye msaada zaidi yako.
Anakuwa na upendo wa muda tu. Anapokuwa na mahitaji, anakukaribia sana; mahitaji yakitoweka, anakutoweka pia.
Utafiti wa Harvard (2020) uligundua kwamba asilimia kubwa ya ndoa zinazovunjika ndani ya miaka mitano huwa zimejengwa juu ya "kuhitajiana" kuliko "kupendana kwa dhati".
Follow na share kwa wengine ๐ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s)
๐๐๐๐๐๐๐