𝗢𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗡 𝗙𝗔𝗖𝗧
𝗢𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗡 𝗙𝗔𝗖𝗧
May 23, 2025 at 02:16 PM
Kupendwa kunajenga misingi ya: i/ Uaminifu ii/ Kujitolea iii/ Uvumilivu Kuhitajika kunapoteza mvuto wake pale ambapo unashindwa kutimiza kile ulichokuwa unatoa. Mapenzi ya kweli hayaegemei kile unachotoa, bali ni wewe kama mtu mzima mwenye thamani yako. Unajuae Kama Unapendwa Au Unahitajika Unatakiwa kujiuliza Je, mtu huyu yuko upande wangu hata nikishindwa? Je, anaonyesha kujali kuhusu hisia zangu au anajali anachopata kutoka kwangu? Je, akipata mtu mwingine bora kwangu kifedha, kimuonekano, atabaki au ataondoka? Katika dunia ya leo yenye misukosuko mingi ya maisha na mahitaji ya kila aina, ni rahisi kujikuta katika mahusiano ya KUHITAJIKA kuliko ya KUPENDWA. Lakini fahamu hivi. Kuhitajika ni mzigo, kupendwa ni baraka. Jenga mahusiano yanayotokana na moyo, si kutokana na maslahi ya mtu. Na wewe mwenyewe, jipime je, unapenda au unahitaji? Kwa wale wanaoamini maandiko. Kasomeni *(1 Wakorintho 13:4–8)* _"Upendo huvumilia, hufadhili, hauhusudu, haujivuni, haujitakasi, haukasiriki upesi, hauhesabu mabaya… Upendo hauishi_ **Quran kasome Surat Ar-Rum (30:21)* _"Na miongoni mwa Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao, naye ameweka baina yenu mawaddah (mapenzi) na rahmah (huruma). Hakika katika haya zimo Ishara kwa watu wanaofikiri."_ Maana yake nini pendo la kweli halitokani na maslahi, bali ni la *kiroho, kihisia na kiutu.* Upendo wa kweli unaendana na utulivu wa nafsi, heshima, na kujali sio tu kutimiza mahitaji bali kuonyesha huruma na uvumilivu. Follow na share kwa wengine 👉 [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s)
❤️ 🫡 2

Comments