𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧
𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧
May 24, 2025 at 03:22 AM
πŸ’ž *MKE WAKO KIPENZI CHA MOYO WAKO.* πŸ’ž > OTHUMAN FACT CHANNEL Katika Kitu Kidogo Mno na Chepesi Mno Kukiteka na Kukimiliki Kwa Mwanaume Mwenye Kujitambua ni Moyo na Upendo wa Mkewe. Sababu,,Hauhitaji Vikubwa wala Vyenye Gharama ili Ufurahi Bali Huhitaji Vidooogo Vyenye Thamani Ndani ya Moyo na Wala Havihusishi Gharama ya Mfukoni. Kwa MUME Ambae Haoni Kamwe Hatoiona Thamani na Wala Hatojali Kukithamini Kitakachomthaminisha Mke Wake. Wala Kushughulishwa na Vyenye Kumpa Furaha Mke Wake. 'Mkeo Tamaa yake Si Pesa,,,Bali Tamaa yake ni Thamani ya Moyo wake na Mapenzi yako juu yake. Na Ukimnyima Thamani yake Usishangae Akahamia Kwenye Pesa Zako,,Ambazo Umezipa Muda Mrefu Kuzitafuta Kuliko Kuitafuta Furaha Yake. Uthamini Moyo Wake,,Atakuthamini na Atavithamini Vyote vya Kwako wala Hatoviharibu wala Kuvisambaratisha. Mpe Upendo Mke Wako,,,Atakufunulia Ukurasa Wake wa Upendo Kwani Mke Wako Ana Upendo Mwingi wa Dhati na Ufunguo wa Ukurasa Huo wa Upendo wake ni Upendo wako. Mpende Atakupenda. Mpe Muda Wa Kuwa Na Wewe,, Nae Ataupa Muda Moyo wako na Mapenzi yako Katika Moyo wake,,,Na Ataupa Thamani yake Stahiqi Ukiumia Naye Ataumia,,Ukihuzunika naye Huhuzunika. Msikilize Mkeo Naye Hatoacha kukusikiliza Wala Kudharau Mazungumzo yako. Hata Ukihisi Wewe ndio Unaongea vya Maana Basi Jua Kama Humsikilizi Mkeo Hayo Maneno yako Kwake ni Pumba Tu Mke Hulipiza Tabia yako. Mfanye Kuwa Rafiki yako Cheza nae Taniana nae Furahi na Utafurahika USO wake na Kukinai Moyo wake na Kujaa Upendo wake juu YAKO na Huzidi Thamani yako Katika Moyo wake. Mahabbah_Yako. Ni Zawadi na Chakula cha Moyo wa Mkeo Mlishe Usimuache Njaa. Follow na share kwa wengine πŸ‘‰ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s) Nawatakia ndoa yenye furaha...❀❀❀
❀️ 😭 3

Comments