
๐ข๐ง๐๐จ๐ ๐๐ก ๐๐๐๐ง
May 25, 2025 at 06:27 AM
*Hakuna hekima ila ni upumbavu unaotokana na ujinga kwa mtu kujivisha mkanda mnene wa UNAFIKI na MAJIVUNO wakati wa uchumba na urafiki wa kimapenzi.*
> OTHUMAN FACT CHANNEL
*Unasimika msingi wa uongo katika maisha yako ya ndoa, unajifanya kuwa una kile ambacho kimsingi hauna kabla au wakati wa uchumba.*
Hauwezi kuuficha Ukweli milele.
Kuna mambo ambayo unaweza kuyaficha wakati wa uchumba, lakini ndoa itayafichua. *Sasa kwa nini ujisumbue?*
Unakopa nguo, viatu, gari, hata nyumba ili tu kumvutia mtu.
Unadanganya kuhusu jina lako, asili ya familia yako, kiwango chako cha elimu, mahali unapofanya kazi, eeh jamani, haumwogopi hata Mungu wako?
*Unadanganya adi chakula unapenda kinabadilika ghafla kutoka maharagwe kwenda pizza.๐คฃ*
Mtu ambaye hujawahi hata kula pizza maishani mwako Leo unasema *"chakula changu pendwa ni pizza na hot dog",* ilhali unapenda furu na supu ya mboga, hot dog ikuchome mdomo huko, ๐
Mwingine utasikia anaanza kuongea Kiingereza cha kifalme, *"in it, in it"* ๐คฃ๐คฃ
Mwisho wa siku Lahaja ya Kimarekani inawaangukia ghafla kama vazi la Eliya
*Wengine wanadanganya hata kuhusu hali zao za usichana/usafi (tazama huyo), na baadhi ya kidada wanaaki kabisa, makalio, mapaja, kama bajeti ya taifa ilivyopakiwa, na kuingia katika ndoa ya kupakiwa, itakayovunjika kwa namna ya kupakiwa hutoamini... Kilichovuta na kumfanya akupende sio uharisia, kafata big nyash anakuja kukutana na small nyash ๐คฃ.*
Kitu kimoja unatakiwa kujua kuhusu Uongo na unafiki huu wote, Vyote vina muda wake wa kuisha....(expiredate๐ญ)
Huwezi kudanganya milele, ukweli utakapofichuka, nini kitatokea? Ushajiuliza au ndo unajiandaa maisha yako yote yawe ni maisha ya udanganyifu, kila siku uwe ni wakutafuta Uongo mpya Ili Mahusiano yenu Yaendelee???
*Suluhisho bora hapa ni Kuhuwa halisi, na kuwa wewe mwenyewe.*
Mtu anayekupenda atakupenda tu.
Mungu alipanga hivyo kwamba vile vitu ambavyo unavionea aibu, ndivyo vinavyomvutia huyo msichana au mvulana kwako.
*Hauhitaji Kuwa Mkamilifu Ili upendwe kikamilifu.*
"Watu hawakupendi kwa sababu wewe ni mkamilifu,
Wewe unakuwa mkamilifu kwa sababu wao wanakupenda."
*Epuka tamaa ya kudanganya wakati wa uchumba, utakuwa unatoa taarifa za uongo kwa mtu anayekupenda, na hilo lazima liwe na madhara mwishowe...*
Ndugu Yangu Mwanaume,
Kama ni gari tu huna kwa sasa, kuna dada huko nje ambaye atakupenda na kuwa na wewe kwa furaha, usijaribu kujifanya kuwa usivyo.
Dada Yangu,
*Hata kwa hilo tumbo lako ambalo limegoma kuwa flat hata baada ya mazoezi mengi makali ya kupunguza mwili, bado kuna mwanaume atakayekupenda hivyo hivyo Ulivyo mpaka ushangae.*
*MUWE NA JUMAPILI NJEMA*
Follow na share kwa wengine ๐ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s)

โค๏ธ
2