
๐ข๐ง๐๐จ๐ ๐๐ก ๐๐๐๐ง
May 25, 2025 at 06:52 AM
*Katika mahusiano au Ndoa unahitaji sana Nguvu ya Mungu ili kudumu*
Ukija huku na mtazamo wa kutaka kila kitu kila wakati kizunguke na kuegemea upande wako na matakwa yako tu, utaharibu jambo.
Itakubidi ujitese mara kadhaa ili kuhakikisha uhusiano unampa nafasi na faraja mwenzi wako pia.
Kuingia katika mahusiano au ndoa bila kuwa na uwezo wa kunyumbulika na kuwa tayari kujirekebisha ili mahitaji na asili ya mwenzi wako yapate nafasi ya kuonekana na kuridhika, ni sawa na kuiua hiyo ndoa/uhusiano kabla hata haijaanza.
Kusema kwamba
"Sipendi kutoka nje na siwezi kubadilika" haitafanya kazi mtu wangu.
i/. Mimi sio wa kupiga simu sana"
ii/. Mimi sio wa kuzungumza sana...
iii/. Mimi sio... Mimi sio..
iv/. Ndivyo nilivyo tu, mimi...
v/. Sio hivyo ninavyopenda..
Mchele au Maharage.
Taa ziwe zimewashwa au zimezimwa. Dadeki
*Katika uhusiano au ndoa, unalazimika kujifunza/kufundwa na kujitolea kupokea mambo mapya na tabia mpya, na pia kuachana na baadhi ya mambo na tabia zako za zamani Ili uendane na mahitaji ya ndoa.*
Usije na fikra zilizoganda kama unataka uhusiano au ndoa yako iwe bora.
Elewa, na jifunze, kunyumbulika.
*WEWE SIO MNARA.*
Follow na share kwa wengine ๐ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s)

๐
โค๏ธ
4