
๐ข๐ง๐๐จ๐ ๐๐ก ๐๐๐๐ง
May 27, 2025 at 01:40 PM
Mhh, Alikuja kuniomba ushauri.
Mwalimu, Niko na mchumba wangu ni miezi miwili Sasa, lakini ananiuliza kama mimi ni bikira.
Anasema anataka kujua kama ataweza kumuoa bikira au la. Ana maana gani kuniuliza kuhusu hali yangu ya ubikira?
Nilimjibu hivi, Mwambie wewe sio bikira, nikamjibu (hata kama dada huyo alikuwa bikira kweliโฆ)
Mwambie ilikuwa ni mara moja tu nimetembea na mwanaume, kosa, na tangu hapo umejitunza. Jibu lake litakupa majibu aliyoyataka, nikamshauri.
Akaenda kufanya kama nilivyomwelekeza.
"Alisema nini?" nikauliza aliponitumia ujumbe wa Habari za jioni Mwalimu siku iliyofuata.
"Mwalimu, huwezi amini, aliniita majina ya kila aina, eti mimi ni malaya, kwamba sikuweza hata kujitunza nikasubiri ndoa, ndio maana sikutaka kumjibu mapema aliponiuliza, alikuwa amekasirika sana.
Nikamjibu, Sasa umeshajua kwa nini aliuliza. Hatua inayofuata ni juu yako mwenyewe.
Ndugu yangu hata wewe,
Nimesikia umeapa kwamba ni lazima uoe bikira, ni bikira hakuna ndoa kabisa.
Sawa tu, Kuwa na matamanio hayo sio mbaya.
Lakini kwanini hutaki kumruhusu Mungu akuongoze, kabla ya kuanza kutumia bikira kama kipimo chako?
Yeye amwonaye mke, amepata kitu chema na ameipata kibali kwa Mungu, siyo Yeye amwonaye BIKIRA. Hata sijuhi kama umenieleza kabisa.
Kuna mabikira unaweza kuwapata na ikawa shida kubwa kwako uwenda shetani kaingilia kati matamanio yako, na wapo mabinti wasiokuwa mabikira utakaowapata na utapata kibali kutoka Muumba wako na kinyume chake inaweza kuwa kweli.
Tuelewane vizuri, simaanishi kukuambia kwamba hufahi kumuoa Bikira HAPANA!!
Kila mtu ambaye bado ni bikira aendelee kujitunze hivyo hivyo ni jambo la kheri na la heshima, kwo na ndo kusudio Kuu la Mungu.
Lakini bikira haipaswi kuwa kipimo ambacho wewe kama mwanaume (au mtu yeyote) utakitumia kupima uwezo wa mwanamke na kumpa kibali Cha kwamba anakufaa kwa ajili ya ndoa ama hafahi.
Ubikira wake utaisha usiku mmoja tu wa harusi,
Lakini TABIA yake na UCHA MUNGU wake (au kutokuwa nao) vitadumu zaidi...
(Hata wewe Leo hii unayesisitiza kuwa ni lazima awe bikira, je wewe ni bikira kweli ndugu?)
Follow na share kwa wengine ๐ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s)

๐
๐ฎ
2