๐—ข๐—ง๐—›๐—จ๐— ๐—”๐—ก ๐—™๐—”๐—–๐—ง
๐—ข๐—ง๐—›๐—จ๐— ๐—”๐—ก ๐—™๐—”๐—–๐—ง
May 30, 2025 at 10:21 AM
*NDOTO SI KIBALI CHA WEWE KUPUUZIA ZAKE โ€” Dada, AMKA* Dada Ninajua uliota ndoto. Uliota kuwa anakuvisha pete. Ukaamka na moyo wako ukaamini kabisa, *Huyu ndiye.* Ukaanza kumuita *My futureโ€ฆ* Ukaanza kujiaminisha kuwa Mungu amenena juu yako. Tafadhaliโ€ฆ AMKA. Tazama tabia yake. Jihadhari usihadaiwe na ndoto, maono, au hisia zinazopambwa, kusababishwa na upweke wako. Dada, Ulisema Mungu alikuambia huyo ndiyeโ€ฆ Sasa mbona anakulazimisha mfanye ngono kwanza? Mbona anakukera, anakuudhi, anakuumiza, lakini bado unasema ni *mapenzi ya Mungu?* Hayo ni mapenzi ya Mungu au ni hisia zako na tamaa zinazokuchezea kichwani? Mapenzi ya Mungu ndo anataka yaanze kwa kutenda dhambi? Kabla ya ndoa, tayari ashaanza kukupiga makofi. Kabla ya ndoa, tayari ameshakufanya utoe mimba. Kabla ya ndoa, unashindwa kulala kwa amani ni presha na huzuni. Hiyo kweli ni baraka kutoka kwa Mungu? Au ni mapigo yaliyojificha? Dada, Ndoto Hazitoshi. Ndoto zinaweza Kuwa ni Ndoto za kawaida, Malaria imepanda kichwani, Njaa kali, Mawazo ya mchana yaliyoingia usiku, Au ni mtego kutoka kwa shetani Usiyaweke maisha yako yote katika majaribu kwa msingi wa ndoto. Angalia alama nyekundu. Chunguza mwenendo wake. Sikiliza maneno yake. Tambua nia yake. Na linganisha na mwongozo wa Maandiko maana yanatufundisha kuwa wale wanaomcha Mungu hujihifadhi na machafu, na hutenda kwa hekima, si kwa haraka. Mapenzi ya kweli hayaji Kwa kivuli cha dhambi. Hayaji kwa kulazimishwa. Hayaji kwa vitisho na ukatili. Hayaji na huzuni ya moyo kila wakati. Hayaji kwa maneno matamu na matendo machafu. *Usiite sumu kuwa ni baraka kwa sababu uliota ukiikunywa na kupona.* Ndoto si sababu ya kuingia kwenye mateso. Mapenzi ya kweli huja na amani, si majeraha. Dada, jifunze kutofautisha hisia na ufunuo wa kweli. Na ukiona uhusiano unakupeleka mbali na maadili KATAA, TOKA, OKOA NAFSI YAKO. Follow na share kwa wengine ๐Ÿ‘‰ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s)
๐Ÿ‘ ๐Ÿ‘ 4

Comments