
๐ข๐ง๐๐จ๐ ๐๐ก ๐๐๐๐ง
May 30, 2025 at 08:11 PM
*Ukomavu Wako ndo Utamlinda Mkeo*
Kama Mwanaume Unapaswa ujue jambo hili mapema
*Kama Mama yako au Ndugu yako hampendi Mke wako, ni lazima uwe mkomavu wa kutosha kushughulikia hali hiyo kwa hekima.*
Hekima, sio kuwa na upendeleo. Ulinzi, sio kuwa na ukatili. Uthabiti, sio wewe Kuwa kimya.
*Wewe ni KIONGOZI wa nyumba yako. Na kama kiongozi, unawajibika kuwalinda wote walioko chini yako, na Mke wako yuko kwenye mstari wa mbele wa ulinzi huo.*
Mume wa kweli, Hamlindi Mke wake tu dhidi ya watu wa mbali. Ila hata familia yake mwenyewe, akiona hawamtendei haki. *Na pia hamruhusu Mke wake kuwaonea familia yake bila sababu.*
Haki ni haki haijalishi upande gani upo.
Kama mwanaume, Usiwe mpole kupita kiasi kwa familia yako wakati wanamtukana au kumdhalilisha Mke wako. Usiwe kimya wakati Mama yako anamnyanyasa Mke wako. *Usiyafumbe macho wakati Dada yako anamwita Mke wako majina ya ajabu na ya kejeli.*
Ukimya wako ni ruhusa kwao kuendelea kuyafanya. Kutokujali kwako ni chombo cha mateso kwa mke wako.
Unajua ni kwanini?
*Kwa sababu wanaamini hutawazuia. Na hilo linawafanya waone huna msimamo, huna uamuzi wewe ni mtoto"wao bado.*
Uwanaume wako hautambuliwi Kusema tu Mimi ni mwanaume.
๐ง๐พ Ndevu hazikufanyi kuwa mwanaume.
Hata kijana wa miaka 17 anaweza kuwa nazo.
Umri haukufanyi kuwa mwanaume. Unaweza kuwa na miaka 40 lakini bado ukawa na akili ya miaka 15 kwenye ndoa.
*๐ต Pesa hazikufanyi kuwa mwanaume. Kuwa na gari, nyumba na biashara hakumaanishi kuwa una uwezo wa kuiongoza familia na ukawa na hekima.*
Ukomavu ndio unakufanya kuwa mwanaume wa kweli.
Ukomavu wa kiroho
Ukomavu wa kihisia
Ukomavu wa kifamilia
Ukomavu wa uamuzi
*Mwanaume wa kweli anapaswa kuwa mlinzi wa familia yake.* Mwanaume wa kweli anajua mipaka ya Mama na Mke.
*Mwanaume wa kweli anasema, Hili si sahihi hata kwa familia yake mwenyewe.*
Na mwanaume wa kweli anajua, Wote wawili wanastahili heshima Lakini Mke wake anapaswa kuwa wajibu wake wa kwanza.
Follow na share kwa wengine ๐ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s)

๐ฏ
1