𝗢𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗡 𝗙𝗔𝗖𝗧
𝗢𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗡 𝗙𝗔𝗖𝗧
May 31, 2025 at 12:33 PM
UNAJUA KABISA UNA MATATIZO, HALAFU HUTAKI KUBADILIKA? Ni UKATILI. Ndiyo, ukatili. Kuwa na uelewa kamili kwamba una tabia, hulka, au matatizo ya kitabia ambayo yatamuumiza mwenza wako siku moja… na Bado ukaamua kutofanya chochote kuyashughulikia. Wewe bado hujaoa au kuolewa, lakini tayari unajua una: ☑️ Hasira za haraka ☑️ Hofu ya karibu au kutokuamini mtu ☑️ Kinyongo cha zamani ☑️ Matatizo ya kiakili au kihisia ☑️ Matatizo ya kifamilia ambayo yanaathiri mitazamo yako ☑️ Matumizi mabaya ya pesa ☑️ Addictions (ulevi, ponografia, nk) ☑️ Tabia ya kukataa kusikiliza ☑️ Matatizo ya mawasiliano Lakini unayafumbia macho. Unasema, “Nitabadilika tu nikisha oa/nikiwa kwenye ndoa. Hilo ni janga. Wale wa Nichague jinsi nilivyo Samahani, hatutakuchagua kwa jinsi ulivyo. Kama tabia zako zinaumiza, Kama zinachosha,. Hatutasujudu kwa kasoro zako kwa kisingizio cha ndivyo ulivyo. Mapenzi sio msumeno wa kusafishia makosa ya muda mrefu. Ndoa sio rehab ya mtu aliyeamua kuzoea mapungufu ya roho Yako. Mume/mke siyo "therapist wa kulazimishwa." Ni uonevu na ukatili kumleta mtu kwenye maisha yako bila juhudi zako za kubadilika. Nini unajua kuhusu nafsi yako, lakini umekuwa ukikwepa kulikabili? Nani ameumia kabla kwa sababu ya hali hiyo? Na ni kwa nini unaendelea kuliacha liwepo? Mapenzi ya kweli hayajengiwa juu ya matumaini ya kubadilika, ila juhudi ya kweli ya mabadiliko. Hakika Mwenyezi Mungu habadilishi hali ya watu mpaka wabadilishe yale yaliyo katika nafsi zao. Kabla hujapendwa, jipe kwanza nafasi ya kupona. Kabla hujaitwa mke au mume, kuwa mtu anayestahili majina hayo. Maana kupendwa na mtu ni neema, lakini kumuumiza mtu aliyeamua kukupenda ni dhambi. Follow na share kwa wengine 👉 [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s)
Image from 𝗢𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗡 𝗙𝗔𝗖𝗧: UNAJUA KABISA UNA MATATIZO, HALAFU HUTAKI KUBADILIKA?  Ni UKATILI. Ndi...
👍 😮 2

Comments