๐—ข๐—ง๐—›๐—จ๐— ๐—”๐—ก ๐—™๐—”๐—–๐—ง
๐—ข๐—ง๐—›๐—จ๐— ๐—”๐—ก ๐—™๐—”๐—–๐—ง
June 2, 2025 at 10:12 AM
USIMPENDE MTU KWA KILE ANACHOKUONYESHA TU Moyo wa binadamu wakati mwingine unakuwa na sura mbili tofauti. Leo anaweza kukuambia anakupenda, lakini ndani yake ana mpango tofauti kabisa. Anaweza kukutumia maneno mazuri, lakini moyo wake upo kwa mtu mwingine tofauti. Usimpende mtu kwa kile anachokuonyesha tu. Mpende mtu kwa kile unachogundua kwa muda, kwa tabia zake, maamuzi yake, na mwenendo wake unapimtazama Wengi leo katika mahusiano yao wameanguka kwa sababu walivutiwa na, Sura nzuri, Maneno matamu, Picha za mtandaoni, vizawadi, na aina ya vitendo vya kuwalaghai vilivyotumika kuziteka hisia zao kwa muda mfupi. Lakini hawakujua kuwa hayo yote yalikuwa kama sinema, *Muigizaji mzuri haonyeshi UKWELI, anaonyesha UJUZI.* Usiyaruhusu mapenzi yakupofushe kutoona alama nyekundu. Ushindwe kumtazama, Anayekuzingua, anayekuficha, Anayekutumia, Anayekudharau, Anayekufanya uhisi kuwa unajilazimisha ...lakini bado unamuita YULE NI WANGU. Mapenzi ya kweli hayafichwi, hayachanganyi, hayapotoshi. Mapenzi ya kweli, Yana uwazi, Yana uthibitisho, Yana heshima, Yana thamani. "Na kama mnapenda kitu na kumbe ni shari kwenu, na mnakichukia kitu na kumbe ni kheri kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui. Surah Al-Baqarah Siyo kila anayekufurahisha leo ni wa kukufaa kesho. Siyo kila anayejifanya kukuona leo, atakuthamini baadae. Fungua macho ya moyo wako. Mapenzi ya kweli hayabahatishwi, unayagundua tu kwa kuiona thamani na nafasi yako kwa mtu husika. Na kama hutaki kuumia kesho jifunze kwanza kuyatazama mahusiano yako kwa macho ya kiroho. Usiweke moyo wako kwa mtu kwa sababu alikuletea zawadi, Weka moyo wako kwa mtu kwa sababu unayaona matendo ya dhati kila siku hata hata hasipoongea Bado unaiona nafasi yake katika Maisha Yako. Follow na share kwa wengine ๐Ÿ‘‰ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s)
๐Ÿ™ ๐Ÿ‘ ๐Ÿง  5

Comments