๐—ข๐—ง๐—›๐—จ๐— ๐—”๐—ก ๐—™๐—”๐—–๐—ง
๐—ข๐—ง๐—›๐—จ๐— ๐—”๐—ก ๐—™๐—”๐—–๐—ง
June 3, 2025 at 10:40 AM
Upepo hauna sura, hauna rangi, hauna umbo lakini kila mtu anaujua ukipita. Kwa sababu una ATHARI. Una nguvu ya kuacha alama, hata bila ya kuonekana. Upepo unatikisa matawi. Upepo unatimua mavumbi. Upepo unabadilisha mwelekeo wa bendera n.k. Hata kama hauonekani, uwepo wake hauwezi kupotea. Na wewe unaweza kuwa hivyo. Usihangaike kuonekana kama wengine wanavyopenda kujionyesha. Jitahidi kuacha alama. Fanya mema kimya kimya, lakini yaache yatikise matawi ya maisha ya watu. Usiseme sana, acha matendo yako yaongee. Usijionyeshe sana, acha athari yako iwaonyeshe wewe ni nani. Usitafute kutambuliwa kwa maneno tafuta kutambuliwa kwa mabadiliko unayoweka. Kuwa kama upepo hauna shepu, lakini una nguvu ya kubadilisha mazingira. Follow na share kwa wengine ๐Ÿ‘‰ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s)
Image from ๐—ข๐—ง๐—›๐—จ๐— ๐—”๐—ก ๐—™๐—”๐—–๐—ง: Upepo hauna sura, hauna rangi, hauna umbo lakini kila mtu anaujua ukip...
โค๏ธ ๐Ÿซก 2

Comments