
๐ข๐ง๐๐จ๐ ๐๐ก ๐๐๐๐ง
June 6, 2025 at 12:41 PM
*HUWEZI KUJENGA IMANI (TRUST) KATIKA MAHUSIANO/NDOA BILA KUWA NA HIVI VITU MUHIMU*
1) UWAZI (TRANSPARENCY)
Huwezi kuwa unaIficha simu yako kwa mwenzi wako halafu unategemea aamini kuhusu wewe, Inaingia akilini kweli? Si hiyo ni juju sasa? Simu yako ina nywila nyingi kuliko benki. Histori ya simu na ya mtandao unafuta kila mara. Unaficha mambo kutoka kwake. Mpenzi wako anapaswa kujua karibu kila kitu kukuhusu, mipango yako, na harakati zako.
Kama unajibu maswali yake kama vile mtu anayepigwa risasi, IMANI hiyo itatoka wapi?
2) UADILIFU / UAMINIFU (INTEGRITY / FAITHFULNESS)
Unataka mpenzi wako akuamini? Zungumza ukweli na timiza unachoahidi. Timiza ahadi zako. Kuwa mwaminifu kwa mpenzi wako, ndipo atakapoweza kusema kwa kujiamini, *Ninamuamini mume/mke wangu.*
Kila mara unapomsaliti mwenzi wako, unaharibu uaminifu wake kwako.
3) KWELI (TRUTH)
Inashangaza jinsi kizazi chetu kinavyoishi kwa uongo kama kapackage Fulani hivi kakuendeshea Maisha Yao. Kuanzia umri wako, muonekano wako hadi hali yako ya kifedha yote ni uongo.
Unaishi wapi? Unadanganya.
Unafanya kazi gani? Uongo tena.
Kila mara uongo wako unapogunduliwa, hata ukweli wako unakuwa hauaminiki tena. Uaminifu bado ni sera bora zaidi. Usidanganye kuhusu maisha yako ya zamani au ya sasa kwa mwenzi wako ukweli ukifichuka, hatakutrust tena.
Husije kutulilia ukiona mwenzi wako hawezi kukuamini. *JICHUNGUZE KWANZA.*
Follow na share kwa wengine ๐ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s)
โค๏ธ
๐
๐ช
๐
4