
๐ข๐ง๐๐จ๐ ๐๐ก ๐๐๐๐ง
June 8, 2025 at 12:09 AM
*Ukiona mtu anakutuliza hasira zako, anakusikiliza bila kukuhukumu, anakushauri kwa upole hata ukiwa kwenye makosaโฆ huyo mtu ni zawadi ya Mungu maishani mwako.*
Siku hizi watu wanapenda kusikika kuliko kusikiliza. Wanapenda kuhukumu kuliko kuelewa. Wanapenda kuongea kuliko kujifunza. Ndiyo maana watu wengi wanapoteza watu wa maana kwa sababu ya ubinafsi, majivuno na ukosefu wa ustahimilivu.
*Usimchukulie poa mtu anayekuelewa ukimya wako. Mtu anayejua umeumizwa hata bila kusema. Mtu anayejua kutuliza mawazo yako bila kutumia pesa wala ahadi. Mtu anayekupenda kwa namna ambayo haikufanyi kujishusha ili umpendeze.*
Mahusiano hayahitaji watu wakamilifu, yanahitaji watu wawili walioko tayari kukua pamoja, kuelewana, kusameheana na kusaidiana kuvuka vipindi vigumu bila kushutumiana. Siyo kila mtu anayekupenda anafaa kuwa nawewe. Bali kila mtu anayekujali kwa vitendo, kukuthamini kwa moyo na kukupa amani, huyo anastahili nafasi yako.
*Acha kuendekeza mahusiano ya muda mfupi yenye kelele nyingi na bado yanashusha thamani yako. Tafuta mtu anayeupa moyo wako utulivu, siyo anayekuchosha kwa drama zisizoisha.*
Follow na share kwa wengine ๐ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s)

๐
โค๏ธ
4