
๐ข๐ง๐๐จ๐ ๐๐ก ๐๐๐๐ง
June 9, 2025 at 05:56 AM
Kabla hujajitoa kwa mtu, mwangalie vizuri kwanza. Sio kwa hayo macho yako ya mapenzi yaliyojaa mahaba mazito juu yake, ila mtazame kwa jicho lenye hekima. Mapenzi sio Kila wakati yatakuonesha Ukweli, lakini hekima ndo itasababidha kuiona kona iliyofunikwa na mihemko Mapenzi.
Umsipende mtu kwa sababu anakufurahisha, mpende mtu anayekujenga. Furaha ni ya muda, lakini inajengwa na uwekezaji wa maisha. Kuna aina ya watu kazi yao ni kuwaletea vicheko maishani mwao, lakini pia wanaleta maumivu ambayo ni ngumu kusahaulika maishani, kwa sababu ya vicheko walivyowahi kutupatia.
Iangalie tabia yake anapokasirika, siyo anapocheka. Angalia anavyokuzungumzia unapokosea, siyo anavyokusifia unapomfurahisha. Angalia anavyoshughulika na matatizo, siyo anavyokushika mkiwa faragha.
Mtu sahihi si yule anayekufanya ujisikie vizuri tu, bali ni yule anayekusaidia kukuwa na kuwa bora zaidi. Anakusukuma kwenda mbele, anakushauri kwa upendo, anakusamehe unapokosea anakusikiliza na kukupa Muda wake.
Mtu sahihi hataki uigize ili umpendeze. Anakukubali na mapungufu yako, anakuheshimu hata akiwa na nafasi ya kukudharau, anakuchagua kila siku hata akiwa na sababu ya kuacha.
Kabla hujajitoa, jiulize: huyu mtu akigeuka upande wa pili wa sarafu, bado nitaweza kuvumilia? Kama jibu ni hapana, chukua muda, tafakari, na usihukabidhi moyo wako mapema Kwa mtu hasiyeijua thamani yako.
Follow na share kwa wengine ๐ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s)
