
๐ข๐ง๐๐จ๐ ๐๐ก ๐๐๐๐ง
June 10, 2025 at 07:08 AM
*Ndoa nyingi hazikuvunjika kwa sababu walisalitiana, ila kwa sababu tu walipoa kihisia. Walianza na mihemko, wakawasiliana kila saa, wakatamani kuwa pamoja kila wakati. Lakini kadri miaka ilivyopita, mazungumzo yanapungua, ukaribu unapungua, hadi sasa ni jina tu limebakiwa Kuwa nyinyi ni wapenzi.*
Upendo haumalizwi na muda, ila unaisha kwa kutowekeza ndani yake. Huachi kupenda ghafla, unaanza kwa kupuuzia, kutojali, na kubeba kila jambo kimazoea. Kila siku unakosea bila kuomba msamaha, kila siku unakwazika na husema, hadi nafsi inachoka taratibu.
Ndiyo mtu uliyemuoa ni yule yule, lakini upendo ndani yake ni tofauti. Sio kwa sababu amebadilika, ni kwa sababu mmeshindwa kuwekeza kwenye penzi lenu. Mlikuwa marafiki, sasa ni washirika wa majukumu tu, watoto, kodi, chakula na usingizi.
Kama upendo umeisha, hauwezi kurudi kwa miujiza. Unahitaji juhudi. Rudisheni mazungumzo. Anzeni kuonana tena, siyo tu kwa kupishana chumbani. Mpe mwenzako muda, jicho la faraja, na neno la kumtia moyo hata kama hakuna jambo kubwa.
Upendo unaishi kwenye mambo madogo, kwa mazungumzo, Kwa kupeana umuhimu.
Ukiitaka ndoa iwe na upendo, acha kutegemea hisia pekee ake. Fanya maamuzi ya kila siku kupenda, kusamehe, kuvumilia, nk. Upendo unaishi kwa vitendo. Na kama mlishapendana kweli, bado mna nafasi ya kupendana tena zaidi, na kwa kina zaidi.
Follow na share kwa wengine ๐ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s)
