๐—ข๐—ง๐—›๐—จ๐— ๐—”๐—ก ๐—™๐—”๐—–๐—ง
๐—ข๐—ง๐—›๐—จ๐— ๐—”๐—ก ๐—™๐—”๐—–๐—ง
June 11, 2025 at 06:37 AM
*Haupo tayari kupenda mtu mpya kama bado una hasira na mtu wa zamani. Haupo tayari kuanza ukurasa mpya kama bado unayasoma kwa siri maumivu ya ukurasa wako wa jana. Haupo tayari kupewa upendo mpya kama bado hujajifunza kujipenda mwenyewe.* Wengi wenu mnaingia kwenye mahusiano mapya mkiwa mmejaa majeraha. Mkitegemea mpendwe hadi mpone. Lakini ukweli ni kwamba, haifanyi kazi hivyo. Mtu anaweza kuwa anakupenda kwa dhati kabisa, lakini kama moyo wako bado una makovu ya zamani, utamchukulia kama adui mpya wa makosa yako ya zamani. *Kuuponya moyo wako sio kusahau yaliyotokea. Ni kukubali kuwa yalitokea, na bado una thamani. Ni kuona nyufa za moyo wako na bado ukajiamini kupenda tena, kwa hekima zaidi.* Wakati mwingine unahitaji kuwa peke yako ili ujue thamani yako haiko kwa mtu mwingine. Ipo ndani yako. Unapojifunza kutabasamu ukiwa peke yako, ndipo unakuwa tayari kutabasamu na mwingine bila kumtumia kama fimbo ya kusahau maumivu yako. *Jiponye. Zungumza na nafsi yako. Yaendee taratibu mambo yako. Hujachelewa. Upendo wa kweli hautokei tu kwa haraka, unaanza kwa yule mtu aliyepona, aliye huru, aliye tayari kupokea bila shaka na kutoa bila woga.* *Moyo uliopona hauna chuki, hauna shinikizo, hauna kiburi. Unapenda kwa dhati. Na unapendwa kwa Kuthaminiwa.* Follow na share kwa wengine ๐Ÿ‘‰ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s) โ™ก ใ…ค ย  ย  โŽ™ ย  โŒฒย ย ย ย ย  ๐Ÿ”• *สณแต‰แตƒแถœแต—ย ย ย  หขแตƒแต›แต‰ ย ย ย  หขสฐแตƒสณแต‰ย ย ย  แต˜โฟแตแต˜แต—แต‰ แถœสฐแตƒโฟโฟแต‰หก*

Comments