
๐ข๐ง๐๐จ๐ ๐๐ก ๐๐๐๐ง
June 11, 2025 at 03:01 PM
Hili nishawahi kulizungumzia sehemu nilisema hivi ๐Sio kawaida, na si salama. Kwa Mtu ambaye aliwahi kuingia kwenye moyo wako, akayajua mapungufu yako, akashiriki nawewe hisia zako hawezi kuwa tu rafiki wa kawaida. Hisia hazina swichi ya kuzima na kuwasha, zinahitaji umbali na muda Ili kupoa.
Kama kuna mtu anaamini kuwa anaweza kuendelea kuwa karibu na ex wake huku akiwa kwenye mahusiano mapya, basi ajue kuwa anachochea moto taratibu. Kuna sababu ya kwa nini mliachana, na kuna heshima inatakiwa kwa yule aliyechukua hiyo nafasi mpya kwenye maisha yako.
Mpenzi wako wa sasa anahitaji usalama wa hisia zake. Anahitaji kujua kwamba moyo wako haujaathiriwa na kumbukumbu za zamani. Anahitaji uhakika wa kwamba hakuna mtu mwingine anayejua upande wako wa ndani kiasi kile ex wako anavyojua.
Kwa sababu ya mtoto, Ndiyo, ni sahihi kuwasiliana hilo ni la lazima. Lakini mazungumzo yao yafungwe ndani ya mipaka ya malezi ya mtoto tu. Kuendeleza stori za kawaida kana kwamba ni marafiki wa karibu, hasa mbele ya yako wewe mpenzi sasa, kunaleta hisia za kutoheshimika, kutothaminiwa, na hata kuleta wasiwasi na mashaka yasiyo ya lazima.
Mwanaume mwenye nia njema anatakiwa kuweka wazi mipaka hiyo na kuilinda ili kulinda amani, uaminifu wa hisia za mwenzi wake wa sasa.
Follow na share kwa wengine ๐ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s)
โก ใ
ค ย ย โ ย โฒย ย ย ย ย ๐
*สณแตแตแถแตย ย ย หขแตแตแต ย ย ย หขสฐแตสณแตย ย ย แตโฟแตแตแตแต แถสฐแตโฟโฟแตหก*
