
๐ข๐ง๐๐จ๐ ๐๐ก ๐๐๐๐ง
June 11, 2025 at 03:41 PM
Sio wewe peke yako wanafamilia wengi wanaingia kwenye hali hii kwa sababu ya *emotional sacrifice* kujinyima kwa ajili ya watoto wapate utulivu wa familia. Ninachoweza kukuambia kwa Sasa ni kwamba *hao watoto hawahitaji tu wazazi wawili walioko chini ya paa moja, wanahitaji amani ndani ya hilo paa.* Watoto wanahisi huzuni ya mzazi aliyejeruhiwa hata kama hakuna kelele. Maisha ya kujibana kihisia yanakuathiri afya ya akili, furaha, na hata malezi yenyewe.
Kiroho, hii ni vita ya ndani. Unaishi na mtu ambaye moyoni huwezi kumwamini, lakini unapaswa kushika amani kwa ajili ya watoto. Hapo ndipo neema ya Mungu ina kazi kubwa maana kwa nguvu zako hutaweza. Inahitaji kuomba kila siku Mungu akupe utulivu wa moyo, hekima ya kukaa kimya pale panapostahili, na ujasiri wa kusimamia ukweli.
Hekima ya kuishi na msaliti ni hii, mlinde mtoto asiwe mwathirika wa chuki zenu. Jenga maisha yako kwa maombi, usikubali heshima yako ipotee kwa sababu ya msaliti, lakini husiwasababishie watoto majeraha ya ugomvi au laana ya kurithi migogoro yenu. Kama unaweza kukaa kwa amani kwa ajili ya malezi, basi fanya hivyo. *Omba Mungu akupe nafasi, muda na uamuzi wa kihekima kwa wakati sahihi.* โ
Follow na share kwa wengine ๐ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s)
โก ใ
ค ย ย โ ย โฒย ย ย ย ย ๐
*สณแตแตแถแตย ย ย หขแตแตแต ย ย ย หขสฐแตสณแตย ย ย แตโฟแตแตแตแต แถสฐแตโฟโฟแตหก*

โค๏ธ
1