
𝗢𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗡 𝗙𝗔𝗖𝗧
June 12, 2025 at 12:45 AM
Natamani ningekujua wewe Ili nikusaidie zaidi Lakini ngoja nikueleze hii kama Bado wewe huna mtoto maana yake Unapooa mwanamke mwenye mtoto, unakuwa baba kabla ya Kuwa baba, unawajibika Kumzaa mtoto huyo, bila kujali kama ni wa kwako au la.
Kama baba wa mtoto huyo bado yupo na anahusika, utakumbana na changamoto ya mipaka, mawasiliano, migogoro ya muda baina ya mtu na mzazi mwenzie hutokwepa hii. Lazima uwe na uvumilivu wa hali ya juu sana. Na kuna wakati utajihisi kana kwamba upendo wa mwanamke huyo unagawanyika kati yako na mtoto, hasa katika miaka ya mwanzo ya ndoa. Hapa lazima uwe na moyo wa uelewa.
Kabla ya kuingia katika ndoa hii hakikisha unao utayari kuanzia wa kiakili pamoja na wakihisia, mtoto hata kama sio wa damu yako, lakini unatarajiwa umlee kama wako. Kama moyo wako hauna nafasi hiyo, usiingie kwenye hiyo ndoa.
Na uangalie uhusiano wao na baba wa mtoto ukoje? Hili ni muhimu sana. Kama bado kuna mawasiliano ya kimapenzi au migogoro isiyoisha, utakuwa katikati ya vita visivyo vya kwako na huna maamuzi juu ya vita hiyo. Na vipi kuhusu, mtoto mwenyewe anakuchukuliaje? Kabla ya ndoa, angalia namna mtoto kukuchukulia. Usipuuze hisia ya mtoto, inaweza kuivuruga au kuisaidia ndoa yako.
Je, unampenda mwanamke huyo kwa dhati? Sio tu kwa sababu ni mrembo na mpole. Lazima uwe na upendo wa kweli ambao uko tayari kupokea mzigo wake wowote. Na vipi yeye anakuona wewe kama baba bora kwa mtoto wake? Si kila mwanamke mwenye mtoto yuko tayari kumkabidhi mwanaume jukumu la ulezi. Hakikisha na yeye yuko tayari kwa hilo, muwe na makubaliano kabla.
Kumuoa mwanamke mwenye mtoto ni wito. Lakini si kila mwanaume anayeweza kubeba huo wito ni wale waliokomaa kiakili, kiroho, na kiupendo. Kama uko tayari kumpenda yeye na mtoto wake bila ubaguzi, Mungu atakubariki sana. Lakini ukitumbukia humo kwa hisia tu bila maandalizi unaweza kubeba msalaba usio wa kwako kwa machungu yasiyoisha.
Omba Mungu akupe hekima, usikurupuke. Na ukishaamua, simama kama baba halali. Mbinguni wanasema *ametimiza agano la upendo.😂*
Follow na share kwa wengine 👉 [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s)
♡ ㅤ ⎙ ⌲ 🔕
*ʳᵉᵃᶜᵗ ˢᵃᵛᵉ ˢʰᵃʳᵉ ᵘⁿᵐᵘᵗᵉ ᶜʰᵃⁿⁿᵉˡ*
