KitaaCtics: Where the Elite Meets The Streets
KitaaCtics: Where the Elite Meets The Streets
May 20, 2025 at 02:14 PM
SI MBAYA KUJUA Singapore ni mojawapo ya miji ya kisasa zaidi duniani inayotumia teknolojia ya hali ya juu kama vile sensa na akili bandia (AI) kusimamia trafiki, kupunguza taka, na kuokoa nishati.  Kwa mfano, zaidi ya asilimia 80 ya makutano ya barabara nchini Singapore yanasimamiwa na mifumo ya AI inayoweza kurekebisha taa za trafiki kwa wakati halisi kulingana na hali ya barabara, hivyo kupunguza msongamano na muda wa kusafiri kwa wastani wa *asilimia 30.* Aidha, mifumo ya AI hutumika katika usimamizi wa taka kwa kutumia sensa katika mapipa ya taka ili kuonyesha ni lini yanapaswa kuondolewa, hivyo kupunguza gharama na matumizi ya mafuta . Katika sekta ya nishati, Singapore imewekeza katika gridi za umeme zinazotumia AI kusambaza nishati kwa ufanisi zaidi na kupunguza upotevu wa nishati . Upo?..
Image from KitaaCtics: Where the Elite Meets The Streets: SI MBAYA KUJUA   Singapore ni mojawapo ya miji ya kisasa zaidi duniani...

Comments