
TRA TANZANIA
May 19, 2025 at 01:26 PM
CG MWENDA HAPOI, ATEMBELEA KIWANDA CHA SIGARA TCC PLC
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda amefanya ziara katika kiwanda cha Sigara Tanzania cha TCC PLC Jijini Dar es Salaam Mei 17.2025 na kujiridhisha kwamba uzalishaji unaofanyika unaendana na kiwango cha Kodi inayolipwa na kiwanda hicho.
Akiwa kiwandani hapo Kamishna Mkuu ametembelea maeneo ya uzalishaji na ufungashaji wa Sigara na kufanya kikao na Uongozi wa TCC PLC ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bw. Roy Manalili.
Kamishna Mkuu Mwenda ameupongeza uongozi wa TCC PLC kwa kuendelea kulipa Kodi kwa hiari na kuwaahidi ushirikiano katika masuala ya Kodi pamoja na utoaji wa Elimu ya Kodi.
Kwa upande wake Bw. Roy Manalili amesema wataendelea kulipa Kodi kwa hiari na kueleza kuwa wamekuwa wakizalisha stiki za Sigara bilioni 6.5 kwa mwaka na wametoa ajira nyingi zikiwemo za wauzaji wa jumla 1,500 na wasambazaji 105,000.
Mwisho

👍
🙏
😮
❤️
😂
😢
24