
TRA TANZANIA
317.1K subscribers
Verified ChannelAbout TRA TANZANIA
TRA Official WhatsApp Channel
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

#KIGOMA Leo tarehe 12 Juni 2025, Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kigoma, Bw. Beatus Nchota, ametembelea Kiwanda cha Qilin Cement kilichopo mkoani Kigoma na kufanya mazungumzo na Kiongozi wa kiwanda hicho, Bw. Fan Junping pamoja na watumishi wengine. Ziara hiyo imefanyika katika mwendelezo wa Kampeni ya Elimu na Utatuzi wa Changamoto za Kodi iliyoanzishwa rasmi tarehe 06 Juni, 2025 na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda sambamba na maadhimisho ya Alhamisi ya Kusikiliza Changamoto za Walipakodi. Katika ziara hiyo, elimu juu ya kodi mbalimbali kama vile VAT, PAYE, Income Tax na nyinginezo imetolewa ikiwemo kusikilizwa kwa changamoto zinazomkabili Mlipakodi na kupatiwa ufumbuzi.


#MBEYA Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo 12 Juni, 2025 imeendelea na kampeni ya utoaji elimu kwa Mlipakodi mlango kwa mlango kwa Wafanyabiashara wa maeneo ya Mwanjelwa, Kabwe na Mwenge ambapo Wafanyabiashara katika maeneo hayo wamehimizwa kwenda kulipakodi awamu ya pili, kufanya usajili wa TIN pamoja na utoaji wa risiti halali za EFD.
