
TRA TANZANIA
May 19, 2025 at 06:22 PM
WAFANYABIASHARA GOBA WAOMBWA KUTOA USHIRIKIANO KWA TRA
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Kikodi Tegeta Bw Dickson Qamara amewataka wafanyabiashara wa Goba kutoa ushirikiano kwa maafisa wa TRA wanaopita katika maeneo yao ya biashara kwa lengo la kutoa elimu ya kodi na kusikiliza changamoto zao kwa lengo la kuboresha huduma zao.
Bw. Qamara ameyasema hayo leo tarehe 19.05.2025 alipokutana na maafisa watakaoshiriki zoezi hilo la mlango kwa mlango ofisini kwake Tegeta, jijini Dar es Salaam.
Bw. Qamara amewashukuru walipakodi kwa kuendelea kulipa kodi vizuri akiahidi kuendelea kuboresha huduma zao ili kurahisisha ulipaji kodi wa hiari.
Nae Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi ambae ni kiongozi wa timu hiyo CPA Paul Walalaze amesema katika zoezi hilo wamejipanga kuwaelimisha wafanyabiashara juu ya mambo mbalimbali ya kodi kama vile usajili wa biashara, wajibu wao wa kutoa na kudai risiti za EFD, kufanya makadirio na kufanya malipo ya kodi ya awamu ya pili.
👍
🙏
❤️
😮
19