Sekretarieti ya Ajira
Sekretarieti ya Ajira
May 20, 2025 at 10:49 AM
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bi. Lynn Chawala, ameambatana na maofisa wa taasisi hiyo kutembelea Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kampasi ya Dodoma. Ziara hiyo imelenga kutoa elimu kwa umma kuhusu mchakato wa ajira serikalini na kuwaelekeza wanachuo juu ya namna bora ya kujiandaa na fursa za ajira. Katika mazungumzo yake na wanachuo wa CBE, Bi. Chawala amesisitiza umuhimu wa kufahamu taratibu za ajira na kutumia vyema mfumo wa Ajira Portal, ambao unarahisisha upatikanaji wa nafasi za kazi katika utumishi wa umma. Wanachuo walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali kuhusu uombaji wa kazi na vigezo vinavyotumika katika mchakato wa ajira, huku wakielekezwa hatua za kuchukua ili kuwa tayari kwa soko la ajira. Serikali inaendelea na jitihada za kuhakikisha vijana wanapata uelewa sahihi kuhusu fursa za ajira, huku taasisi husika zikiendelea kuelimisha jamii ili kuongeza uwazi na ufanisi katika utoaji wa ajira serikalini.
Image from Sekretarieti ya Ajira: Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, Sekretariet...
👍 😢 ❤️ 💩 😭 🙏 17

Comments