START TEK
START TEK
June 3, 2025 at 02:56 PM
🚨 JE, UNAJUA JINSI AKAUNTI ZA WHATSAPP HUWA ZINAIBIWA? Ukiwa hujajua, kuna mbinu hatari zinazotumiwa kuiba akaunti za WhatsApp – na mara nyingi huonekana ni kawaida, lakini zina madhara makubwa sana. Hebu tuangalie: 🔍 1️⃣. SIM SWAP SCAM Mhalifu anapata taarifa zako (jina, namba ya simu, ID n.k.), kisha anaenda kwa kampuni ya simu kuomba SIM mpya akidai umezama au kupotea. Akifanikiwa: 📩 Atapokea SMS zako, ikiwemo WhatsApp verification code na kuiba akaunti yako. 🧠 2️⃣. SOCIAL ENGINEERING ATTACK Hii ni mbinu ya kukudanganya utoe code ya WhatsApp: ❗ Unapokea SMS yenye 6-digit code 📞 Halafu unapigiwa simu au kuandikiwa DM ukidanganywa kuwa ni WhatsApp au kampuni fulani 😱 Ukitoa hiyo code – akaunti yako imekwenda! 🖥️ 3️⃣. WHATSAPP WEB HIJACK Mtu akifikia simu yako kwa sekunde chache, anaweza ku-scan QR code kwa WhatsApp Web na akaanza kusoma chats zako zote bila wewe kujua. 🧪 4️⃣. MALWARE / LINKS ZA KUDANGANYA Ukibofya link za ajabu kwenye SMS, WhatsApp au email – zinaweza kuingiza malware kwenye simu yako na kufungua njia kwa mhalifu kuiba taarifa zako. ✅ JINSI YA KUJILINDA: 🔐 Washa TWO-STEP VERIFICATION: WhatsApp > Settings > Account > Two-step verification > Enable ❌ Usiwahi kumpa mtu code ya WhatsApp ⚠️ Epuka kubofya link usizozijua 👀 Thibitisha mara mbili mtu anayedai anatoka kampuni fulani 🔧 Unahitaji msaada kuwasha Two-step Verification au kukagua usalama wa WhatsApp yako? 👇 Tuma ujumbe sasa: 📷 Instagram: @prime_persuits ✉️ Email: [email protected] Elimu ya kidigitali ni silaha bora dhidi ya uhalifu wa mtandaoni. Sambaza ili wengine wajifunze pia! 📲💡 — #digitalsecurity #primepursuits #cyberawareness #internerbundle

Comments