
START TEK
June 11, 2025 at 08:33 AM
FAIDA ZA LIPA NAMBA KWA MFANYABIASHARA.
1. Kutoa Pesa Bure kwa Wakala ✅.
Hutalipa gharama yoyote unapotaka kutoa pesa kupitia wakala yeyote Tanzania nzima.
2. Kuondoa Usumbufu wa Chenji 💵.
Mteja analipa kiasi kamili unachodai bila kutegemea chenji, biashara yako inakuwa ya uhakika na yenye weledi.
3. Kuongeza Ulinzi wa Hela 🔐.
Ukishapokea malipo kupitia lipa namba, mteja hawezi kurudisha pesa kama ilivyo kwa laini za kawaida.
4. Kupunguza Hatari ya Chuma Ulete🚫.
Kukosa pesa mkononi hupunguza uwezekano wa hasara za kishirikina kwenye biashara.
5. Kutuma Pesa Benki Bila Malipo 🏦.
Unaweza kuhamisha pesa kwenda kwenye akaunti ya benki moja kwa moja bila gharama yoyote.
6. Kupokea Malipo Kutoka Mitandao Mbalimbali📲.
Mteja wa mtandao wowote anaweza kukulipa kwa urahisi.
7. Kuzuia Hasara ya Kutembea na Pesa Cash 🛡.
- Kupunguza hatari ya kuibiwa au kupoteza pesa ukiwa safarini.
Elimu kwa Mfanyabiashara:
Lipa namba ni mfumo salama wa kisasa unaokusaidia.

💼
🤑
2