SITTA SPORTS ARENA
SITTA SPORTS ARENA
June 9, 2025 at 01:34 PM
*NI VITA YA KUMWANIA ZUBIMENDI⚽👇* Kiungo wa kati wa Real Sociedad, Martin Zubimendi yupo karibu zaidi kujiunga na klabu ya Arsenal licha ya ripoti mbalimbali kuhusu Real Madrid kutaka kuingilia kati uhamisho wa Fundi huyo kutua North London, taarifa za kukamilika kwa dili hilo zimesambaa kwa wiki kadhaa sasa lakini hakuna upande wowote umethibitisha si mchezaji wala klabu hiyo. Kiungo huyo wa kati raia wa Hispania mwenye umri wa miaka 26, alionesha kiwango bora sana kwenye mchezo wa fainali ya UEFA Nations League hapo jana akifunga goli moja kwenye sare ya 2-2 huku wakipoteza Ubingwa huo kwa Ureno kupitia mikwaju ya penati. Ubora huo wa Zubimendi umezua minong'ong'ono kuwa huenda uhamisho wake kwenda Arsenal ukakwama, ikisemekana Real Madrid tayari washaanza harakati za kupata huduma ya Fundi huyo wameripoti Diario AS, Jarida maarufu nchini Uhispania likidai kuwa Real Madrid wanapanga jaribio la mwisho la kuteka nyara uhamisho huo na kumleta kiungo huyo Bernabeu majira haya ya Joto. SITTA SPORTS UPDATES ⚽
Image from SITTA SPORTS ARENA: *NI VITA YA KUMWANIA ZUBIMENDI⚽👇*  Kiungo wa kati wa Real Sociedad, M...

Comments