SITTA SPORTS ARENA
SITTA SPORTS ARENA
June 11, 2025 at 11:01 AM
MABOSI wa klabu ya Hassania Agadir ya Morocco 🇲🇦 wapo katika mazungumzo ya kuipata saini ya kiungo nyota wa Simba raia wa DR Congo, Fabrice Ngoma, huku taarifa zikielezwa mchezaji huyo huenda akajiunga na kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao. Ngoma aliyejiunga na Simba Julai 14, 2023, akitokea Al Hilal ya Sudan, mkataba alionao na kikosi hicho cha Msimbazi unafika tamati Juni 30, 2025 na hadi sasa hakuna mazungumzo ya kuongeza mwingine jambo linalotoa nafasi ya kusepa kikosini. Taarifa kutoka Morocco, zinaeleza viongozi wa Hassania Agadir, wako hatua nzuri za kuipata saini ya nyota huyo kwa ajili ya msimu ujao, huku suala la masilahi binafsi baina ya klabu hiyo na mchezaji hayawezi kuleta shida kwa siku za karibuni. Kituo kikubwa cha Radio Mars cha Morocco, kimefichua viongozi wa Hassania wako hatua za mwisho za kuipata saini ya kiungo huyo kwa ajili ya msimu ujao, huku masilahi binafsi sio kikwazo kwao na kuanzia muda wowote dili hilo linaweza likakamilika. Arena inatambua nyota huyo alitaka kuondoka dirisha dogo lililofungwa Januari mwaka huu, ingawa ushawishi wa Kocha Simba, Fadlu Davids ukambakisha kutengeneza kikosi bora na cha ushindani katika Ligi Kuu na michuano ya kimataifa ya CAF, Simba ikifika fainali ya Shirikisho.

Comments