
SITTA SPORTS ARENA
June 11, 2025 at 11:42 AM
BAADA ya kuwepo kwa tetesi za muda mrefu Yanga kuhitaji huduma ya kiungo mshambuliaji wa Tabora United, Offen Chikola inadaiwa amemalizana na klabu hiyo kwa kupewa mkataba wa miaka miwili, ikiwa na maana msimu ujao ataonekana na uzi wa vijana wa Jangwani.
.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga kinasema kuwa, Chikola aliyeitibulia watetezi hao wa Ligi Kuu kwa kufunga mabao mawili wakati wanaizamisha kwa mabao 3-1 katika mechi ya mkondo wa kwanza, ameshasaini mkataba huo wakati anasubiri dirisha lifunguliwe atambulishwe.
.
Katika msimu huu Chikola kafunga mabao saba, washindani wake wa namba ambao anakwenda kukutana nao Yanga, Maxi ana mabao matano, asisti tisa na Mzize ana mabao 13 na asisti tatu, hivyo ushindani utakuwa mgumu.
.
“Yanga tuna mchakato wa kukifumua kikosi chetu, kuna wachezaji ambao watapelekwa kwa mkopo kama Farid ndio maana Chikola anaingia, kuna wengine ambao wamemaliza mikataba yao kama kiwango chao hakikuisaidia timu watapewa mkono wa baibai,” kilisema chanzo changu na kuongeza:
.
“Lakini wapo wachezaji waliomaliza mikataba bado wanahitajika na timu, hao tutakaa nao mezani kufanya mazungumzo ya kuwaongezea mipya na tayari tumefanya hivyo kwa baadhi yao kama Nzengeli na Dickson Job.”