
SITTA SPORTS ARENA
June 11, 2025 at 11:53 AM
*CITY YATAMBULISHA BEKI KISIKI ⚽*
Manchester City imemsajili beki wa kushoto *Rayan Aït-Nouri* kutoka Wolves. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Algeria amejiunga na City ili kuongeza ushindani na nguvu kwenye nafasi ya beki wa kushoto.
Aït-Nouri anajulikana kwa kasi, uwezo wa kushambulia kutoka nyuma, na uwezo mzuri wa kiufundi. Usajili huu unaimarisha zaidi kikosi cha Pep Guardiola kuelekea msimu mpya, na unampa chaguo lingine muhimu kwenye safu ya ulinzi.
SITTA SPORTS UPDATES ⚽
