
TRT Afrika Swahili
May 19, 2025 at 08:50 AM
Mwenyekiti wa chama cha upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu, mapema hii leo amefikishwa katika Mahakama ya Mkazi ya Kisutu iliyopo jijini Dar es Salaam.
Lissu anakabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwemo la uhaini.
Viongozi mbalimbali, kutoka chama chake cha Chadema, pamoja na baadhi ya wanaharakati kutoka nchini Kenya wamehudhuria kesi hiyo.
Awali kumekuwa na taarifa za kuzuiwa kuingia nchini Tanzania kwa baadhi ya wanasheria na wanaharakati kutoka Kenya na hatimae kurudishwa nchini mwao.
Aliyekuwa waziri wa katiba Kenya Martha Karua pamoja na mawakili wengine walizuiliwa kuingia Tanzania siku ya Jumapili.
Jumatatu Jaji Mstaafu wa Kenya Willy Mutunga na wanaharakati wengine walirudishwa nyumbani.
Lakini jaji mwingine mstaafu wa Kenya David Maraga aliruhusiwa kuhudhuria kesi ya Tundu Lissu jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, serikali ya Tanzania, bado haijatoa ufafanuzi wa sakata hilo.
