
JamiiForums
June 8, 2025 at 11:21 AM
DAR: Baadhi Waumini wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania (Kanisa la Ufufuo na Uzima) linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima ambalo Juni 2, 2025 lilifungiwa na Serikali, wamejitokeza eneo la pembezoni mwa Kanisa hilo lililopo Ubungo wakisali na kuimba nyimbo mbalimbali za Dini
Wakati hayo yakiendelea Kanisa limezungukwa na Askari Polisi ambao wapo tangu siku Serikali ilipotangaza kulifungia Kanisa hilo kwa kutoa huduma kwa kile kilichoelezwa kutoa matamshi ya Kisiasa yenye lengo la kuichonganisha Serikali na Wananchi
Awali, jana Juni 7, 2025, Katibu Mkuu wa Kanisa hilo, Dkt. Erick Shoo alitangaza kutokuwa na ibada katika matawi yao yote Nchini, badala yake ibada zifanyike nyumbani hadi watakapopewa taarifa zaidi
Soma https://jamii.app/WaumiziWaGwajima
😂
👍
😢
🙏
❤️
😮
✌️
👏
📌
62